July 13, 2017

Nguvu ya Maamuzi part 6:Mungu ama shetani
Hizi ni pande mbili zinazokinzana,  mtu yeyote hutakiwa  kuchagua  pande moja wapo. Kila pande ina  aina yake ya maisha.Maamuzi ya kuchagua pande yoyote kati ya pande hizi  yana matokeo yake. Tofauti kubwa ya pande hizi  ni kwamba pande ya shetani  humkubali mtu anayechangamana baina ya pande zote mbili yani upande wa shetani na upande wa Mungu Lakini Mungu kamwe aambatani na mtu  anayechangamana na shetani. kama maandiko yasemavyo “        Hamwezi kushirikiana katika meza  ya Bwana na katika meza ya mashetani. Au twamtia Bwana wivu? Je tuna nguvu zaidi yake?
Kuchagua njia Ya Mungu Ama njia ya Ya shetani  yote ni maamuzi ambayo Mwanadamu huchagua
Warumi 12:1 basi ndugu zangu  nawasihi  kwa huruma  zake Mungu  itoeni miili yenu  iwe dhabihu  iliyohai takatifu  ya kumpendeza Mungu  ndiyo  ibada yenu  yenye maana. Wala msifuatishe  namna ya dunia hii bali mgeuzwe na kufanywa upya nia zenu  mpate kujua  hakika mapenzi ya Mungu  yaliyo mema
  Kuamua kumfuata Mungu ni lazima kuambatane na  na kuutoa mwili kama dhabihu  takatifu  anaposema-Je hamjui kuwa miili yenu ni hekalu takatifu?
-       Maana yake ni kwamba lengo la kwanza la kila kitu kinachousiana na mwili wako Liwe ni kumpendeza Mungu
 Anaposema “mpende Bwana Mungu wako  kwa moyo wako
 wote  kwa akili zako zote”Mathayo 22:37
maana yake -Ufahamu wako na moyo  wako vitumike kufanya yale yampendezayo Mungu

-Kuamua kumfuata Mungu; ni kutokufuatisha  namna ya dunia hii  ama kutoruhusu mfumo wa dunia hii  kutuathili  na kututenga na Mungu  Warumi12:2
-       Kuamua kumfuata Mungu ni kuwa tayari  kugeuzwa  nia zetu  kwa kuruhusu neno La Mungu  kuathili  mfumo  wetu wa maamuzi  ili tumpendeze Mungu kwenye  maamuzi tunayoyafanya Yoshua 1:8
 hebu tafakari maneno haya maandiko yanaposema “mtu atakaye kuiokoa  nafsi yake ataipoteza na mtu atakayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona”  mathayo 16:25
Nafsi hujumuisha ufahamu na akili ya mtu, nafsi hujumuisha hisia  za mwili; kwenye nafsi ndiko tunapata mtazamo wa mtu na namna mtu anavyoyachukulia mambo, hivyo unaweza kuelewa maandiko yanaposema atakaye kuiokoa nafsi yake anamaanisha kwamba atakaye kufuata manufaa ya nafsi yake ataipoteza  mwili una manufaa  na matakwa yake,  kuamua kumfuata mungu ni pamoja na  kukana matakwa ya nafsi yako .
Kuna wakati utatakiwa kwenda kinyume na mtazamo wako, kuna wakati utatakiwa kuzikana hisia zako, kunawakati utatakiwa kuwapoteza baadhi ya rafiki zako,  kwa ajili ya kumfuata Mungu, hivyo ni lazima ujue kwamba kumtumikia Mungu kuna gharama. Kuna mtu alimfuata Yesu akimuomba akamzike kwanza baba yake ndipo amfuate Yesu akamjibu akamwambia waache wafu wakawazike wafu  wewe unifuate mathayo 8:21 ,vivyo hivyo tajiri mmoja alipomuuliza yesu anawezaje kuurithi ufalme wa Mungu  Yesu alijibu akamwambia uza vyote ulivyonavyo ndipo unifuate  Yule tajiri akahuzunika  moyoni kwa kuwa alikuwa na mali nyingi. Marko10:17-22 Maandiko  yanaposema  “njia ya kwenda upotevuni ni njia pana na njia ya kwenda ya kwenda uzimani ni nyembamba tena imesongwa” Mathayo 7:13-14; hii inamaanisha ni jambo rahisi sana kutenda uovu kuliko kutenda haki  hivyo mtu aliyeamua kufuata njia ya haki hupaswa kuwa amefanya maamuzi sahihi ya kujikana. Watu wengi huiendea njia pana kwa sababu ni rahisi tena ina ushawishi mkubwa  kumbuka kuwa tunaishi kwenye dunia ambayo  maandiko yalituambia kwamba ulimwengu unatuchukia sisi Yohana 15;19.  Hi ndio dunia ambayo maandiko yanatuambia “ole wa ulimwengu kwa maana  Yule mshitaki ameshuka kwenu  mwenye gadhabu nyingi akijua kuwa muda wake ni mchache” ufunuo 12:12 tena  maandiko yanatuambia shetani kama simba aungurumaye , akitutafuta ili atumeze.  Kuna wakati Yesu anawatuma wanafunzi wake akawaambia “nawatuma ninyi kama kondoo kati kati ya mbwa mwitu wakali  iweni wapole kama njiwa na wajanja kama nyoka” Yesu akawatahadharisha jinsi ambavyo kuna wakati watawachukua na kuwapeleka mabalazani. mathayo 10:16-18
Kumfuata shetani ni kuongozwa na matakwa ya Mwili
Duniani kuna ushawishi mkubwa wa kuifuata njia ya shetani   ushawishi unaanzia kwenye miili yetu miili yenye  asili ya dhambi iliyojawa na tamaa  na hila za kila namna  maandiko yanatuambia  wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu tena wale waufuatao mwili wanajenga uadui kati yao na Mungu Warumi 8:6-8 Hivyo kumfuata mungu ni kujikana nafsi zetu wenyewe ni kuitoa miili yetu kuwa dhabihu takatifu ya kumpendeza Mungu Tena ni kuifanya miili yetu hekalu  Takatifu
Kuifuata njia ya Mungu kuna majaribu na vikwazo lakini kuna thawabu iliyokubwa sana  Yusufu alidhamilia kuifuata njia ya Mungu hata alipokutana na ushawishi mkubwa hakukubali kumtenda Mungu dhambi Yusufu alisema “Nitafanyaje uovu huu nikamtende Mungu dhambi”mwanzo39:9
Alikuwa tayari kupingana na tamaa ya mwili wake  tena alikubali kuyazuia manufaa ambayo  yanaasili ya dhambi na uasi,  Danieli alitupwa kwenye tundu la simba  kwa kutokubali kuiabudu sanamu wengine walitupwa kwenye tanuru la moto Lakini Mungu aliwatetea kwa sababu ndani yao walidhamilia kumfuata Mungu
Kuamua kumfuata Mungu si kwenda kila jumapili kanisani peke yake
Kuamua kumfuata Mungu si kutoa sadaka na fungu la kumi  peke yake
Si kuwa  mzee wa kanisa tu.
Yesu aliwalinganisha mafalisayo na masadukayo kama  makaburi ambayo yamepambwa kwa nje lakini ndani imejaa mifupa    kwa namna ya nje walionekana kuwa wanamtumikia Mungu kwa uaminifu mkubwa lakini  Yesu alipotazama mioyo yao aligundua kwamba ni wanafiki wakubwa wanafiki kwa sababu wanachokisema hawakifanyi
Maandiko yana sema watu hawa huniabudu kwa midomo lakini mioyo yao iko mbali nami Mathayo 15:8-9
Wakati mwanadamu anahangaika kujionyesha kuwa ni mwema na tena anamcha Mungu mbele za watu Mungu anautazama moyo wake  jinsi anavyomtenda Mungu dhambi akiwa mahali pa sirini  Daudi alipolijua hilo alisema “Ee bwana umenichunguza na kunijua wewe wajua kwenda kwangu na kuondoka kwangu Hamna neno ulimini mwangu usilojua kabisa Bwana” zaburi139:1-4
Kuamua kumfuata mungu ni kuishi mfumo wa maisha ya kumpendeza Mungu bila ya kujali mazingira umpendeze Mungu ofisini umpendeze Mungu nyumbani pia, ukiwa mahali pa jumuia na ukiwa sirini pia
watu wengi tunasema tumeamua kumfuata mungu lakini hata hatujachukua hatua ya kumjua Mungu tuliyeamua kumfuata Mungu  kama maandiko yasemavyo  “nawapenda wale wanipendao nao wanitafutao kwa bidii wataniona” mithali 8:17 
Je umechukua hatua thabiti za kumpenda Mungu na kumtafuta kwa bidii
Je unamjua Mungu unayemwabudu? samweli alikaa hekaruni kwa miaka kadhaa lakini hakumjua Mungu wake;  Mungu alipoita samweli, alikwenda kumuuliza baba yake mlezi Eli kama amemwita, Jiulize je unamfahamu Mungu uliyeamua kumfuata je akiita unaitambua sauti yake? Je akisema na wewe unasikia?  Yohana 8;47 “Yeye aliye Wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu”  uko tayari kuifuata njia yake  na kuyashika maagizo yake? Yohana 8;31 “ ninyi mkikaa katika neno Langu mmekuwa wanafuzi wangu kweli kweli”
Je mnahojiana naye Mungu anasema unikumbushe na tuhojiane  eleza mambo yako upate kupewa haki yako isaya 43:26
Je unamtumikiaje Mungu? Mungu ametuweka sisi kama mabalozi wa siri zake 2wakorintho 5:20 tena amesema kwamba sisi ni watenda kazi pamoja na yeye 1wakorintho3:9  umesimama katika nafasi gani katika kumtumikia Mungu? Manufaa ya kumtumikia Mungu huja tunaposimama kwa uthabiti katika kumtumikia yeye  
Kuamua kumtumikia Mungu kwa dhati kuna faida nyingi sana Yesu anatuambia mtu akinitumikia baba atamuheshimu Maandiko yanasema  Hakuna siraha itakayofanikiwa kwa wale walioamua kutii agizo La Mungu, tena Mungu ameamuru Baraka utabarikiwa mjini na shambani pia, Tena Mungu Ambaye hakutaka kutuacha wapweke akatupatia Roho mtakatifiu Atufundishe na kutuongoza na kututia kwenye kweli yote  haya yote yanawezekana ukiamua kuifuata njia Ya Mungu pia Ukimtumikia Mungu kwa uaminifu.
Kufuata njia ya shetani ni kutafuta uangamivu  wako mwenyewe;Kumbuka jambo ili muhimu kuwa uamuzi uko juu yako ukiamua kufuata njia zako mwenyewe ukaongozwa na mwili wako maana yake umeamua kuifuata njia ya shetani  kwa maana maandiko yamesema yoyote asiyeongozwa na roho wa Mungu huyo si wake  warumi 8:5-9 kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya  mwili –(maana yake huongozwa na matakwa ya miili yao )bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho maana yake- (huongozwa na matakwa ya Roho wa Mungu) kwa kuwa nia ya mwili ni mauti (maana yake kuufuata mwili ni kwaajili ya uangamivu wako mwenyewe  mwili utakuongoza katika mambo ambayo yataharibu mafanikio yatakayokutoa nje ya kusudi la Mungu)bali nia ya roho ni uzima na amani (kuongozwa na roho wa Mungu ni kwa ajili ya uzima wako wewe mwenyewe pia kwa ajili ya amani yako wewe mwenyewe ) kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu kwa kuwa haitii sheria ya Mungu wala haiwezi kutii (kwa maana ingine ni kwamba mwili wa mwanadamu una asili ya dhambi  Mtu anapoamua kuufuata mwili  anatengeneza uadui na Mungu  kwa hiyo Maamuzi ni yako kuufuata mwili kwa kwenda kinyume na sheria ya Mungu Au kuifuata Roho ya Mungu kwa kwenda kinyume na matakwa ya Mwili wako
Yakobo 4:4 “enyi wazinzi  hamjui ya kwamba kuwa rafiki ya dunia ni kuwa Adui wa Mungu basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanyia kuwa adui wa Mungu”  Tangu awali Mungu alimpa mwanadamu maamuzi ya kuamua kufuata njia ya Mungu ama Ya shetani  Mungu anasema nimeweka mbele yako uzima na Mauti  uzima ni kwa kutii Agizo la Mungu na Mauti ni kwa kwenda kinyume na Agizo la Mungu
Unapofanya maamuzi ya kumtumikia Mungu fanya maamuzi ya kweli, Amua Mungu awe kiongozi wa maisha yako, Mungu akuongoze kwa kila jambo  kwako, Unaweza ukawadanganya wanadamu lakini  Mungu anautazama moyo wako.
Watu wengi tunapenda matokeo ya kumfuata Mungu lakini hatutaki kuamua kuishi maisha  ya kumfuata Mungu.
Matokeo huletwa na mfumo , kuamua  kumfuata Mungu ni kuamua kuishi maisha ya  kumpendeza Mungu  hapo ndipo utafaidi  matokeo ya kumfuata Mungu 

Joshua aliwaambia wana wa Israel chagueni hivi leo mtakayemtumikia Lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Mungu. Yoshua24:14-15 Maamuzi yako mikononi mwako ukiamua kumfuata Mungu kubali kutenda matendo ya kumpendeza yeye na kufuata njia zake huu ndio mfumo pekee wa maisha utakaokufanya ufurahie matunda ya kumtumikia Mungu.
Emmanuel Mwakyembe
+255716531353
emamwakyembe@gmail.com