July 25, 2017

Unaifahamu nguzo muhimu kwa mafanikio ya biashara yako?

Kuna mtazamo mbaya kwa watu ambao wako njee na ndani ya biashara kuhusu biashara kwamba ni sehemu ya kufaidika tu wakati wengine wanaumia.

Wanadhani kwamba kwenya biashara unahitaji kuangalia faida tu bila ya kujali mambo mengine yanaendaje.

Ni kweli biashara lazima iwe na faida, lakini kwa mtazamo wa aina hii, wengi wameingia kwenye biashara na kushindwa kufikia mafanikia makubwa kwa sababu wao wanajali faida tu na kuachana na vitu vingine na hata kama wakipata mafanikio, mafanikio hayo niya mda mfupi tu.

Hakuna kitu muhimu kwenye biashara yenye mafanikio ya kudumu kama uaminifu. Biashara zote ambazo unaona zimefanikiwa zimejengwa kwenye misingi ya uaminifu.

Kama umeamua kufanya biashara, jua ya kwamba uaminifu ni kitu ambacho huwezi kucheza nacho hata kidogo. Uaminifu ni nguzo muhimu sana kwenye biashara yako. kwa jinsi utakavyotunza uaminifu ndivyo utakavyoweza kudumu kwenye biashara na kufanikiwa pia.