July 22, 2017

Mistari 7 ya Biblia itakayo kuinua kwenye siku mbaya.

Habari yako? Siku yako ama ya rafiki yako inaendaje? Kama uko vibaya na unahisi mambo yamekuelemea ama hata rafiki yako, si vibaya kuigeukia Biblia, maana ni kitabu ambacho kwetu sisi Wakristo, kinaonyesha njia. 

Mistari yake ina uwezo wa kukubadili na kukufariji pia.

Soma: Mistari 10 ya biblia itakayo kufariji nyakati za upweke.

Hivyo basi kama wewe ama rafiki yako amekuwa na siku mbaya, pitia mistari hii na uitafakari ahadi ya Mungu kwako. John Calahan wa Christian Post amezikusanya.

1 Petro 5:6-7
Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

2 Thesalonike 3:16
Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.

Wafilipi 4:6-7
Msijisumbu kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

Zaburi 50:15
Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza

Mathayo 7:7
Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtaona; bisheni nanyi mtafunguliwa

1 Thesalonike 5:16-18
Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.

Yohana 16:33
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

Tazama Video: Ukiokota pochi au mkoba wenye pesa utafanya nini? Check huyu jamaa alicho kifanya!!