July 23, 2017

Ukiachwa kubali kuachika, acha kumsaidia kupona maumivu ya kukuacha!

 Mwanaume au hata mwanamke anapomuacha mtu, tuseme anapokuacha wewe tena ukiwa hujamfanyia kitu chochote kibaya, hata kama ana roho mbaya kama shetani basi ataumia. Hataonyesha lakini kuna wakati anakaa na kujisikia vibaya kwa kitendo alichokifanya na atajichukia kidogo kwa hilo.

Anaona ulimfanyia wema lakini kakuacha bila sababu tena kwa dharau. Hiki ni kitu ambacho kipo kwa kila mwanadamu, anajisikia vibaya na anaweza hata kuwaza kuwa maisha yake hayatakua sawa kwani ametenda unyama kwa mtu mwema kama wewe. Hatakuambia lakini anahisi hivyo.

 Sasa unapoachwa hembu kubali kuachika, ni sehemu ya kawiada ya maisha. Kutembea na ndugu yake au rafiki yake kutampa hasira za muda mfupi lakini atakusahau na utamthibitishia kuwa kweli alikua sahihi kukuacha kwnai wewe ni Malaya kweli.

 Kwamba kama umeweza kutembea na ndugu yake au rafiki yake basi ungemsaliti kama angekuoa. Lakini yeye atasahau ila wewe hutasahau utaendelea kujiona Malaya na utajiwekea lebo. Kwamba hata mtu siriasi akija kutaka kukuoa akisikia kua ulitembea na mtu na ndugu yake atakukimbia.

 Ndiyo atakuja tu kujua kwani duniani mambo mabaya ndiyo ambayo husambaa na kubaki kirahisi. Hawata kukumbuka kama Binti aliyetumiwa miaka minne na kuachwa kwa dharau. Watakukumbuka kama Malaya aliyetembea na mtu na mdogo wake au mtu na rafiki yake.

 Bila kujua namna ulivyoachwa watamuonea huruma huyo mshenzi aliyekuacha. Watasema Kaka wa watu afadhali wamemuacha, angeoa kimeo yaani kumbe alikua anawachanganya mtu na mdogo wake, mtu na rafiki yake.

 Hawatajua kama ulaichwa kwanza ndiyo uakaamua kulipa kisasi bali watajua ndiyo tabia yako na hutamuumiza yeyote kwa kujitoa kwa mwingine. Trust me ni uamuzi ambao utaujutia milele, kubali kauchika umia kivyako na usilipe kisasi.

 Labda niwaambie kitu mwanaume kama kakucha yeye na hakupendi, wala hatajali unatembea na nani? Lakini anaweza kujali sema kwa muda flani ila baadaye akaona ni upuuzi. Unapotembea na rafiki yake tembea kwakua unataka lakini si kwakua unataka kumuumiza.

 Unajiumiza wewe zaidi kuliko yeye, tena utakua unampa nafuu, kwasababu mwanzoni alipokuacha bila makosa alikua akijilaumu kuwa kakuacha na hujamkosea kitu. Ila ulipotembea na rafiki yake unamuambia hapana hujakosea mimi ni Malaya afadhali umeniacha.

 Yaani kisaikolojia unampa kaunafuu flani, unamsaidia kupona. Hapa nisawasawa na umuibie mtu simu, utajisikia vibaya kwa kuiba lakini ukija kusikia kuwa kumbe hata simu haikua yake nayeye aliiba utapata unafuu kwa kusema wote ni wezi.

Najua inaumiza ila utaumia zaidi kama utautoa mwili wako kwajaili ya kumuumiza. Kwanini aendelee kukuumiza wakati ameshakuacha, hembu leo sema hapana, mimi ni bora zaidi ya hapa, ameniacha lakini nitasimama kwaajili yangu na silipi kisasi cha kijinga.Mwanaume au hata mwanamke anapomuacha mtu, tuseme anapokuacha wewe tena ukiwa hujamfanyia kitu chochote kibaya, hata kama ana roho mbaya kama shetani basi ataumia. Hataonyesha lakini kuna wakati anakaa na kujisikia vibaya kwa kitendo alichokifanya na atajichukia kidogo kwa hilo.

Anaona ulimfanyia wema lakini kakuacha bila sababu tena kwa dharau. Hiki ni kitu ambacho kipo kwa kila mwanadamu, anajisikia vibaya na anaweza hata kuwaza kuwa maisha yake hayatakua sawa kwani ametenda unyama kwa mtu mwema kama wewe. Hatakuambia lakini anahisi hivyo.

 Sasa unapoachwa hembu kubali kuachika, ni sehemu ya kawiada ya maisha. Kutembea na ndugu yake au rafiki yake kutampa hasira za muda mfupi lakini atakusahau na utamthibitishia kuwa kweli alikua sahihi kukuacha kwnai wewe ni Malaya kweli.

Kwamba kama umeweza kutembea na ndugu yake au rafiki yake basi ungemsaliti kama angekuoa. Lakini yeye atasahau ila wewe hutasahau utaendelea kujiona Malaya na utajiwekea lebo. Kwamba hata mtu siriasi akija kutaka kukuoa akisikia kua ulitembea na mtu na ndugu yake atakukimbia.

Ndiyo atakuja tu kujua kwani duniani mambo mabaya ndiyo ambayo husambaa na kubaki kirahisi. Hawata kukumbuka kama Binti aliyetumiwa miaka minne na kuachwa kwa dharau. Watakukumbuka kama Malaya aliyetembea na mtu na mdogo wake au mtu na rafiki yake.

Bila kujua namna ulivyoachwa watamuonea huruma huyo mshenzi aliyekuacha. Watasema Kaka wa watu afadhali wamemuacha, angeoa kimeo yaani kumbe alikua anawachanganya mtu na mdogo wake, mtu na rafiki yake.

Hawatajua kama ulaichwa kwanza ndiyo uakaamua kulipa kisasi bali watajua ndiyo tabia yako na hutamuumiza yeyote kwa kujitoa kwa mwingine. Trust me ni uamuzi ambao utaujutia milele, kubali kauchika umia kivyako na usilipe kisasi.

Labda niwaambie kitu mwanaume kama kakucha yeye na hakupendi, wala hatajali unatembea na nani? Lakini anaweza kujali sema kwa muda flani ila baadaye akaona ni upuuzi. Unapotembea na rafiki yake tembea kwakua unataka lakini si kwakua unataka kumuumiza.

 Unajiumiza wewe zaidi kuliko yeye, tena utakua unampa nafuu, kwasababu mwanzoni alipokuacha bila makosa alikua akijilaumu kuwa kakuacha na hujamkosea kitu. Ila ulipotembea na rafiki yake unamuambia hapana hujakosea mimi ni Malaya afadhali umeniacha.

Yaani kisaikolojia unampa kaunafuu flani, unamsaidia kupona. Hapa nisawasawa na umuibie mtu simu, utajisikia vibaya kwa kuiba lakini ukija kusikia kuwa kumbe hata simu haikua yake nayeye aliiba utapata unafuu kwa kusema wote ni wezi.

Najua inaumiza ila utaumia zaidi kama utautoa mwili wako kwajaili ya kumuumiza. Kwanini aendelee kukuumiza wakati ameshakuacha, hembu leo sema hapana, mimi ni bora zaidi ya hapa, ameniacha lakini nitasimama kwaajili yangu na silipi kisasi cha kijinga.