Featured Posts

July 29, 2017

Umuhimu wa kujenga mahusiano bora na watu wengine.

Binadamu ni viumbe ambao wana mizunguko mingi katika siku zao za kuishi hapa duniani. Binadamu hao hao hukutana na jamii za watu tofauti tofauti katika shughuli mbalimbali za kusaka Mafanikio kama vile mashuleni, kwenye semina mbalimbali na sehemu nyingine mbalimbali.

Binadamu hawa pamoja na kukutana kwako, ni watu wachache hutambua thamani ya kukutana kwako. Hebu tujiulize swali dogo tu, rafiki zako ulikuwa unasoma nao hata kucheza nao leo wapo wapi? Unajua wanafanya nini? Je ni wazima bado au walishafariki siku nyingi na wewe huna taarifa?

Kwa mfano leo hii umekutana na mtu maarafu popote pale, jambo la kwanza utakaloliwaza katika akili yako ni kupiga picha na mtu huyo ili uje uweke mitaandaoni huku ukiandika maneno mbalimbali, kama vile katika ubora wangu.

Ndugu msomaji, kila mtu unayekutana naye, kuna sababu huenda akakusaidia katika safari yako ya mafanikio na sio kupiga picha na kuzidi kuwa na maisha yale yale kila siku.

Kila mtu unayekutana naye kuna sababu. Cha msingi ni kujenga mahusiano bora na mtu huyo. Inawezekana ndiye atayekuwa msaada mkubwa katika kubadilisha maisha yako.

Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao unajiona maisha yako yamebadilika kwa sababu ya mtu fulani ndiye alichangia kuwa hapo ulipo chukua dakika chache kumshukuru huyo aliyekusaidia. Japo wengi wetu hatuna tabia hiyo ya kuwashukuru watu waliotusaidia kufika hapa tulipo, basi ni muda muafaka wa kutoa shukrani.

Jambo la msingi la  kumbukumbuka kila unayekutana naye  kuna sababu hivyo jenga mahusiano na anayekutana naye.