July 14, 2017

Upendo timilifu kwa wanandoa huwa na sifa hizi 3.

Sifa ya kwanza ni tendo la ndoa. Kwamba wapendanao huwa hawana kasoro katika eneo hili. Sifa ya pili ni Ukaribu, kwamba muda wote huwa karibu na kila mmoja hakai na kiu ya kutokumuona mwenzake kiasi cha kupoteza hisia na kushawishika kufanya usaliti.

Isikupite hii: Mambo 10 Mwanaume Anayopenda Kusikia Kutoka Kwa Mwenza Wake.

Sifa ya mwisho ni Kujitolea, ni mahodari kusaidiana, kufarijiana na hawako tayari kupokea mambo kutoka pembeni yanayohusu uhusiano wao, hivyo huwa si rahisi kwao kuyumba kwa sababu za umbea

Kumbuka katika penzi hili tendo la ndoa huwa si sehemu muhimu sana kwa wapenzi, yaani kwao penzi ni rohoni zaidi kuliko mwilini hata wakikaa muda wa miezi mitano bila kufanya tendo la ndoa upendo wao haupungui.

Hata hivyo, penzi la aina hii kwa mujibu wa wataalamu ni vigumu kupatikana na ni vigumu pia kulilinda, lakini linatajwa kuwa ni aina ya penzi bora ambalo ni muafaka kwa maisha ya baadaye ya ndoa kwa wanaopendana.    

Isikupite hii: Je, Ana Upendo Wa Dhati? Mtafunga Ndoa Au Anakuchezea Tu? Mpime Kwa Njia Hizi 8.

Watu wengi kwa kutotambua aina hii ya mapenzi wamejikuta wakiliharibu kwa kufikiri tu kwamba wapenzi wao wamefika na hivyo kufanya makusudi ya kuharibu misingi ya penzi.

"Nimeshamshika atakwenda wapi, nikikohoa tu anaitika" Kauli kama hizi ni hatari sana katika penzi hili, hivyo inashauriwa ukiona unapendwa na mpenzi wako katika aina hii ya penzi ni vema ukawa macho ili kutolivunja kwa uzembe wako na kudhani unababaikiwa kumbe unapendwa kwa dhati.