July 12, 2017

Watoto wanaolaziwa wakiwa na uzito mdogo hawata oa - utafiti.

Kwa mujibu wa tafiti, imethibitika kwamba watoto wa kiume wanaozaliwa wakiwa na maumbo madogo na uzito mdogo, uwezo wao wa kuoa hupungua ukilinganisha na wenzao wenye maumbo makubwa na uzito mkubwa. 

Kulingana na moja ya ripoti iliyotolewa na watafiti wa kiingereza kupitia kwenye jarida la la British Medical, imegundulika kuwa wanaume ambao waliozaliwa wakiwa na maumbo na uzito mdogo, ukubwani huchelewa sana kuoa au hushindwa kabisa kuoa. 

Hata hivyo, kulingana na matokeo ya uchunguzi huo, imebainika kwamba kuna mambo mengi yanayosababishwa wanaume waoe ikiwa ni pamoja na yale ya kibaiolojia na kijamii. 

Na pia imefahamika kwamba, kasoro zinazojitokeza wakati wa kuzaliwa hasa kwa upande wa watoto wa kiume, zinaweza zikapelekea mtu kuwa matatizo makubwa ukubwani

Matatizo hayo ni pamoja na ugumu wa kujumuika na watu wengine, kupungua kwa uwezo wa kujamiiana, matatizo ya kitabia na hasa kihisia na mengineyo. 

Tatizo kubwa liko kwa watoto wakiume wachanga wanaozaliwa wakiwa na uzito unaopungua kilo tatu na nusu. Ukweli ni kwamba watoto wanaozaliwa wakiwa na uzito pungufu na huo, wako katika uwezekano mkubwa wa kushindwa kuoa wanapokuwa watu wazima.