July 28, 2017

Wazazi ndio chanzo cha vijana na watoto kuharibika.

Katika kizazi hiki maadili yameshuka, heshima imeondoka, utii ulishakufa na sasa tunamalizia mazishi yake. 

Ni ukweli usiopingika kwamba matumaini yetu juu ya watoto na vijana wetu wa leo ambao ndio taifa la kesho yameshuka na wengine tayari tumeishakata tamaa, Kwa sababu ya mambo mabaya na ya aibu ambayo watoto na vijana wetu wamekuwa wakiyafanya na kuyaonesha katika jamii yetu. 

Swali kwetu wazazi na jamii kwa ujumla. Je! Ninani wakulaumiwa juu ya haya? Ni wazazi? Jamii? Walimu? Ama utandawazi? 

Tukichimba kwa undani zaidi jukumu la kusimamia, kuangalia na kulea watoto kwanza nila wazazi, hao ndo wanachukua asimilia kubwa katika malezi ya watoto, na watoto wakiharibika lawama na aibu huanzia kwa watoto, kisha kwa wazazi na jamii pia.

Pili walimu na jamii nayo huchangia katika malezi ya watoto kwa asilimia fulani. Ni vigumu na usipo kuwa makini huwezi kabisa kugundua mchango mzuri au mbaya wa malezi utakao kwa walimu mashuleni au jamii.

Kwa upande wangu mimi naona kwamba chanzo cha watoto kuharibika ni sisi wazazi wenyewe.

Siku hizi, wazazi wamekuwa bize, wakitafuta pesa na kumbana na maisha, wanasahau juu ya watoto wao ambao ni wamuhimu na thamani kubwa kuliko hata hizo pesa. 

Imagine wazazi wote hawapo, mtoto yuko nyumbani na house girl ama anazunguka mtaa baada ya mtaa, kwa mtindo huu watoto wetu kwanini wasiharibike? Maana hawana mtu wakusema nao, kuwafundisha ama kuwaonya. 

Kumbuka ni vigumu sana kwa watoto kusikiliza, kuamini na kutii sauti ya house girl (Yaya) au mtu yeyote tofauti na mzazi wake. 

Waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi, watoto hawa wanaokuwa bila kusikiliza sauti ya baba wala mama (mafundisho, maelekzo na kuonywa) baada ya muda mfupi hawataweza tena kusikiliza na kutii sauti za wazazi milele, kwa sababu hawaoni umuhimu na faida zozote za kuwa na wazazi, wanachojua ni kwamba kazi ya baba au mama ni kutafuta na kunipa pesa tu. Ikishafika hatua hii ndo unaona wazazi wanaanza kushituka na kuangahika huku wakilaaumu utandawazi.

Mama anazunguka huku na kule na gari yake, nyumbani amemwacha mtoto wa miezi tisa na house girl akirudi ni saa 2 usiku mtoto alisha lala, Baba ndo hata hajui sura ya mtoto wake.

Utandawazi umeanza kwanza kuwaharibu wazazi na sasa wazazi wanaharibu watoto wao kwa kushindwa kuwapa malezi bora. 

Utandawazi ni koti ambalo wazazi wanatumia kujifunikia baada ya wao kushindwa kuwafundisha, kuwaonya na kuwalea watoto wao katika maadili mema. 

Mtoto yoyote alielelewa na wazazi wake vizuri hawezi kuaribiwa na utandawazi kwa urahisi tu hivi kama ambavyo watu husema kila siku.

Wewe unadhani chanzo cha watoto kuharibika ni nini? toa maoni yako kwa kucomment hapa chini.