Featured Posts

July 29, 2017

Hawa ndio wezi 13 wapumbavu zaidi duniani

Katika karibu kila jambo duniani, mwanadamu huhitajika kutumia akili ili kufanikiwa. Bila shaka, iwapo utatarajia wazidi watu wengine hasa katika kuwapora au kuwaibia basi utahitajika kuwa na ujanja zaidi.

Lakini maeneo mbalimbali duniani kunao wahalifu ambao walionekana kupungukiwa. Majuzi kwa mfano, wanaume wawili kutoka Skegness, Lincolnshire, walijipiga picha wakiimba pesa kutoka kwenye mitambo ya kucheza Kamari Bradford, Uingereza.

Hawakuenda mbali, kwani walikamatwa muda mfupi baadaye Benjamin Robinson, 30, alifungwa jela miezi 32, naye Daniel Hutchinson akahukumiwa kifungo cha miezi sita jela ambacho kimeahirishwa. Hawako peke yao. Hapa ni msururu wa wahalifu wengine waliojichongea: 

1. Jambazi aliyejitapa Facebook.
 Andrew Hennells alikamatwa baada yake kuandika kwenye Facebook akijisifu kuhusu mpango wake wa kushambulia duka la jumla la Tesco eneo la King's Lynn, Norfolk.
Andrew HennellsImage copyrightFacebook Image caption Andrew Hennells aliweka picha yake na ya kisu Facebook Aliweka kwenye Facebook picha yake ya kujipiga yaani ‘selfie’, picha ya kisu na kuandika: "Doing. Tesco. Over." (Nafanya. Tesco. Twende). Alikamatwa na polisi dakika 15 baadaye akiwa na kisu chake na pesa £410 alizoiba. Alifungwa jela miaka minne Aprili mwaka jana. 

2. Mwizi aliyetekwa na usingizi 
Wachumba katika eneo la Lancashire walirejea kutoka likizoni mwaka 2014 na kumpata mwizi amelala usingizi wa pono katika kitanda chao. ChojnowskiImage copyrightAllan Bentley Cavendish Press Image caption Chojnowski alilala kitandani baada ya kufua nguo zake za ndani Martin Holtby and Pat Dyson walishangaa kumpata mwizi huyo Lukasz Chojnowski, alikuwa ameosha vyombo, akafua nguo zake za ndani na hata kununua mboga.
Wanasema nyumba yao haikuwa safi sana walipoondoka kwenda likizoni. Walipata Chojnowski, aliyetoka Poland lakini akahamia Leeds, alikuwa amefanya usafi vilivyo. Chojnowski, 28, alikiri kosa la kuvunja nyumba na akatakiwa kukaa miaka miwili bila kutenda kosa na kulipa gharama ya £200. 

3. Wezi wa penguini 
Watalii wawili kutoka Wales walijipata taabani 2012 baada yao kulewa na kuiba ndege aina ya penguini kwa jina Dirk kutoka kituo cha Sea World, Australia. Rhys Owen Jones, 21, na Keri Mules, 20, waliamka baada ya ulevi kuisha na wakajipata na ndege huyo katika chumba chao. Walijaribu sana kumlisha na kumtunza kwa kumuweka kwenye bafu, mahakama iliambiwa. Baadaye walimwachilia kwenye mtaro. Walionekana na majirani ambao waliwapasha habari polisi na wakakamatwa. Hakimu aliwatoza dola 1,000 za Australia (kiasi sawa na £637) kila mmoja na kuwashauri wasiwe wanakunywa vodka sana. Dirk alirejeshwa Sea World akiwa salama. 

4. Mwizi aliyewatumia polisi picha nzuri 
Mwanamume aliyekuwa akisakwa kwa makosa ya kuteketeza na kuharibu mali alituma picha ya selfie kwa maafisa wa polisi akisema picha iliyotumiwa na maafisa hao katika tangazo la kutafutwa kwake haikuwa ya kupendeza. PughImage copyrightLima Police Department Image caption Picha ya kushoto ndiyo iliyokuwa imetumiwa na polisi.
Aliwatumia iliyo kulia Donald "Chip" Pugh aliwatumia maafisa wa polisi picha aliyojipiga mwenyewe na kuandika ujumbe unaosema: "Hii hapa picha yangu nzuri, hiyo mliyotumia ni mbaya sana”. Polise katika mji wa Lima, jimbo la Ohio, walikuwa wamepakia picha kwenye ukurasa wao wa Facebook wakiomba msaada wa kumtafuta Bw Pugh. Polisi walimjibu na kusema angefanya hisani zaidi kwa kujifikisha kwao. Alikamatwa baadaye jimbo la Florida. Soma zaidi hapa: Mshukiwa anayesakwa atumia polisi 'selfie' 

5. Gaidi aliyejitokeza kudai zawadi 
Maafisa nchini Afghanisan waliachwa vinywa wazi baada ya kamanda mmoja wa kundi la Taliban kujisalimisha na kisha kujaribu kudai zawadi ya $100 iliyokuwa imeahidiwa mtu ambaye andesaidia kukamatwa kwake. Image copyrightNot Specified Mohammad Ashan, alituhumiwa kupanga mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Marekani na Afghanistan mashariki mwa nchi hiyo. Ripoti zinasema alifika katika kizuizi cha polisi mwaka 2012, akaelekeza mkono wake kwenye bango lenye picha yake na kisha akadai zawadi hiyo ya $100. Maafisa wa usalama walishangaa sana na kushindwa kuelezea kitendo chake. Afisa mmoja wa Marekani anadaiwa kuambia wanahabari: “Kusema kweli, mwanamume huyu ni mpumbavu.” 

6. Aliyetishia watu kwa tango 
Mwanamume mmoja alijaribu kuwaibia wacheza bahati nasibu Glasgow kwa kuwatishia akiwanyooshea tango, kwa Kiingereza cucumber.
Gary Rough aliwanyooshea tango hilo likiwa limefunikwa kwa soksi na kudai pesa kutoka kwa mwanamke aliyekuwa kwenye kaunta eneo la Ladbrokes, Shettleston nchini Uingereza. Image copyrightThinkstock Alikabiliwa na kukamatwa na polisi ambaye hakuwa kwenye zamu. Awali, aliambia polisi alikuwa akifanya mzaha, na kisha akawauliza: „Nitaenda jela kwa sababu ya hili?”Alifungwa jela na Mahakama Kuu ya Glasgow 2014 baada ya kukiri kosa la kushambulia watu akiwa na lengo la kuwaibia. 

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.