August 3, 2017

Epuka chuki kwa kufanya haya

CHUKI
Sisi binadamu namna yetu rahisi ya kuelewa na kukumbuka mambo ni kwa kuyaweka mambo katika makundi mfano tunawagawa watu katika makundi kama marafiki, ndugu, watoto, maadui, warefu, wafupi, n.k. 

Makundi haya yanatusaidia kujenga picha ya haraka hata kama wakati fulani hatuwezi kuelezea wazi wazi kundi husika ni nini haswa na pia kunaweza kuwa na tofauti kati ya watu au vitu katika kundi husika.

Isikupite hii: Siri za matajiri wakubwa hizi hapa

Mtindo huu wa kutambua vitu au watu kwa makundi ndio unaopelekea pia kuwepo kitu tuiitacho kwa kiingereza PREJUDICE yaani CHUKI.

Kwakuwa umezoea kuwaweka watu katika makundi fulani, na kuwatambua watu kwa makundi kutokana tayari na aina ya picha ya kundi husika , basi waweza kujikuta ukiwaweka tuu watu katika makundi na kuwatafsiri hivyo, ingawaje sio sahihi kwani ingawaje wewe unafikiria na kutambua kwa njia ya Makundi, kumbuka kuna utofauti mkubwa kati ya mtu aliyepo katika Kundi na maana unayoipa Kundi husika.

Hivyo unaweza kumtafsiri mtu kuwa Mvivu/Mwizi/Mwongo kwa sababu tuu unamuona yupo katika kundi fulani ambalo wewe huwaita wavivu/Wezi/waongo, ila kiukweli huyo mtu mmoja sivyo unavyodhani.


Mara ngapi umesikia mtu akisema "Vijana wa siku hizi wavivu", na wengine wamekosa kazi kwa sababu tuu eti wamemaliza chuo fulani hivyo "hawana ujuzi".

Chuki  ni pale unapowatafsiri watu wengine vibaya kwa sababu kiakili yako wapo katika Makundi ambayo ni mabaya. Unaamini kwa mfano kila anayefanya biashara Online ni tapeli, kila mwenye nayo basi ni tapeli, kila Mnigeria ni mwizi, n.k

Kumbuka ili kuzuia Chuki ya namna hii jitahidi kufikiria na kuwaona watu kama mtu mmoja mmoja na sio sehemu ya kundi.
Kuwa makini na namna unavyotafsiri watu kwa kuangalia Umri , Jinsia, Utaifa, Dini, Kabila, Aina ya kazi, Miji anapotoka, Mahali anapoishi n.k


Isikupite hii: Hizi ni gharama zilizojificha ambazo zinakuzuia wewe kufikia utajiri.

Pia jichukulie wewe ndio ungekuwa una tafsiriwa vibaya ungejisikiaje ?