Featured Posts

August 2, 2017

Ambwene Mwasongwe akemea wahuni wenye hizi tabia.

Kupitia account yake ya Facebook Mtumishi wa Mungu Ambwene Mwasongwe amekemea baadhi ya wahuni wanao-waharibu waimbaji, hasa waimbaji wanaoanza kuchipuka.
"Shalom! Kumekuwa na wahuni wengi siku hizi wanawaharibu watumishi wa Mungu, hasa waimbaji wanaoanza kuchipuka kwa kuwaambia wasiimbe jina la Yesu na wasiimbe maandiko. Eti kwa kisingizio cha kutoka maana watu hawapendi maandiko na hawapendi nyimbo zinazomtaja taja Yesu! Napenda kuwatia moyo waimbaji wote wa injili Tanzania mlioamua kutumika kaeni huu ni wakati sahihi na muhimu sana kuliimba jina la Yesu na kuimba maandiko kuliko wakati mwingine wowote na kila atakayefanya hayo Mungu atamkuza na kumwinua juu sana kuzidi maneno ya hawa wahuni! Pia nawaonya wanaowapotosha waimbaji hawa washindwe kwa Jina la Yesu. Kila atakayepata ujumbe huu amtie moyo mwimbaji wa karibu yake kwa kumwambia Yesu ni jiwe letu la pembeni. Amen" Alisema Ambwene Mwasongwe