August 9, 2017

Dalili 13 za kuvamiwa na mapepo/mtu mwenye mapepo.

Mapepo ni hali ya utendaji kazi wa shetani.
Ni viumbe wa kiroho wanaomwingia mwanadamu na kumfanyisha au kumsaidia kufanya uovu mbele za MUNGU. Ndugu jichunguze na kama una baadhi ya dalili hizi hapo chini hakikisha unavunja kwa maombi mpango huo wa shetani kwa jina la YESU KRISTO(1 Yohana 3:8b) Kwa kusudi hili MWANA wa MUNGU alidhihilishwa ili azivunje kazi za ibilisi.

Isikupite hii: Mistari 7 ya Biblia itakayo kuinua kwenye siku mbaya.

1. Kukosa amani ghafla au kuhisi vitu vinatufanya tuwe na hofu na woga. 
2 Timotheo 1:7 ''Maana MUNGU hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.'', na katika 1 Yohana 4:18 ''Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo''
2. Kukosa uhuru wa kufanya tunavyotaka na kulazimishwa kufanya tusiyotaka kutokana na nguvu fulani kutoka ndani mwetu.  
3. Kuota ndoto usiku ambazo hutufanya tuwe na kichwa kizito sana wakati wa kuamka, kuota majitu ya kutisha kwa namna ya kivuli yakitaka kutukaba au kutudhuru.
4. Kukosa usingizi kabisa na akili yetu kufunikwa na mawazo mfululizo.
5. Vitu kutembea mwilini, kuhisi mwili unawaka moto.
6. Kusahau kusiko kwa kawaida na kuwa na uzito kichwani.
7. Kupiga miayo hovyo tena mfululizo tena bila kuchoka chochote.
8. Kuchukia mme/mke bila sababu yoyote.
9. Hali ya kubebeshwa mzigo kichwani ,kifuani,mgongoni au sehemu nyingine lakini mzigo huo hauonekani kwa macho.
10. Kuwa na hali ya kuogopa vitu vidogo vidogo kama kivuli, au kuogopa kuwa pekeyako chumbani, kuogopa kuvuka daraja au barabara.
11. Kukosa uwezo wa kufikiri, kupenda kuongea wakati wote hata ukiwa peke yako na kukosa kusikiliza wengine. Kuwa na hali ya kulewa bila kunywa kileo chochote.
12. Kwa hali isiyo ya kawaida kuona watu wanakuja kufanya uasherati na wewe ndotoni, kuota unapelekwa porini, kunyweshwa madawa ya uganga ndotoni, pia kuota ndoto za watu waliokufa wakifanya mazungumzo na wewe.
13. Kusisimka mwili ghafla na nywele kusimama.

Isikupite hii: Mistari 10 ya Biblia itakayo kufariji nyakati za upweke.

Ndugu kama una moja ya dalili hizo hakikisha unafanyiwa maombezi na umpokee BWANA YESU maishani mwako ili uwe mbali na uonevu huu wa mapepo ambao ni mawakala wa shetani.