• Isikupite Hii

  August 31, 2017

  Dalili za figo kutokufanya kazi vizuri / kufeli


  Figo zina majukumu muhimu sana katika mwili wa binadamu- kwanza inaondoa sumu kutoka mwili wa binadamu na kusafisha damu na kutoa sumu zote.

  Kama figo haifanyi kazi vizuri, basi hii inaweza kusababisha mkusanyiko wa sumu katika mwili na inaweza kusababisha baadhi ya matatizo makubwa ya afya.

  Isikupite hii: Jikinge na magonjwa ya moyo.

  Dalili za mwanzo za ugonjwa wa figo na jinsi ya kuweka figo zako katika afya nzuri

  Figo inafanya kazi nyingi muhimu katika mwili wa binadamu


  1. Kuweka katika uwiano mzuri kiwango cha maji
  Figo ina uwezo wa kusawazisha kiwango cha maji katika mwili wa binadamu,na pia inashiriki katika kutoa kemikali kwa njia ya mkojo

  2. Kutoa taka mwilini
  Sisi sote tunajua moja ya kazi kuu za figo ni kusafisha mwili, kutoa sumu,chumvi na urea

  3. Kusimamia kanuni za damu
  Kama kiwango cha oksijeni kitakuwa chini katika figo, itasababisha kuundwa kwa erythroprotein, homoni ambayo inachochea marrow katika mifupa(bone marrow)

  4. Kusimamia Kanuni za asidi
  Hii ni muhimu sana katika kazi za figo, figo zinawajibika kwa kuweka uwiano sawa wa asidi katika
  mwili wa binadamu

  Magonjwa ya figo
  Kuna sababu nyingi tofauti zinazoweza kukusababishia ugonjwa wa figo na kushindwa kufanya kazi, magonjwa kama kisukari,ukimwi na shinikizo la damu.

  Tunaweza kusema shinikizo la damu ni moja ya sababu ya ugonjwa wa figo na hii ndio maana inapaswa kujaribu kuweka sukari katika damu na BP katika uwiano wa kawaida.

  Dalili za mwanzo za ugonjwa wa figo

  Kwa bahati mbaya dalili za ugonjwa wa figo zinaanza kuonekana katika hatua za mwisho za ugonjwa,au wakati figo zinakaribia kabisa kushindwa au wakati ambao kuna protini nyingi katika mkojo.

  Kwa kawaida dalili za awali za matatizo ya figo haziwezi kugundulika, ni asilimia 10 tu ya watu wanaweza kujua kama wana ugonjwa wa figo

  Hizi ni baadhi ya ishara za mwanzo za figo kushindwa kufanya kazi


  • Kubadilika rangi kwa mkojo(mfano damu katika mkojo au kwenda haja ndogo mara kwa mara)
  • Uchovu na kukosa nguvu
  • Maumivu ya mgongo hasa juu ya kiuno usawa wa figo
  • Kuvimba miguu au mikono
  • Ukosefu wa umakini na ufafanuzi wa akili
  • Kukosa hamu ya kula na kutokuwa na ladha katika kinywa
  • Kushindwa kupumua vizuri
  • Upele au chronic tingling


  Jinsi ya kuzuia ugonjwa wa figo na kuboresha kazi ya figo yako
  Kama tulivyosema awali,magonjwa ya figo yanaweza kukuletea matatizo makubwa zaidi katika afya zetu.Inatupasa kufanya mabadiliko katika milo yetu na maisha kwa ujumla

  Kipi cha kubadilisha katika mlo?
  Chakula chako kisiwe na mafuta mengi, zuia utumiaji kupita kiasi wa chumvi na potassium, na upendelee kula matikiti maji au apples na katika chakula chako kiwe na kiwango kidogo cha protein. Na pia matumizi ya maji yawe si chini ya glasi nane kila siku

  Mfumo wa maisha
  Pendelea kufanya mazoezi hili kuweka uzito wako vizuri na kupunguza uwezekano wa kupata kisukari,na utapiamlo. Na pia zuia matumizi ya pombe na kuacha sigara

  By Richard Edward

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.