August 4, 2017

Fahamu Mambo 8 kuhusu Train za umeme zinazoletwa Tanzania.

1: Treni itakuwa inasimama kwenye vituo sita kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo itasimama Pugu, Soga, ruvu, Stesheni ya Ngerengere na mwisho Treni itasimama Morogoro.

2: Kutokana na Treni kutumia umeme Serikali imejipanga kutoa umeme wa uhakika kwa 100% na wananchi wasiwe na shaka yoyote kwani umeme wa Treni hujengewa nyaya zake maalum zinazotofautiana na nyaya za umeme wa kawaida.

3: Treni hii itakuwa na uwezo wa kusafirisha wagonjwa mahututi kwani ni za kisasa na zina mwendo wa haraka ambapo itatumia saa moja na nusu kutoka Morogoro hadi Dar es Salaam.

4: Umeme utatumia vyanzo vyenye nguvu kutoa umeme wa Treni kama vyanzo vya maji na makaa ya mawe.

Isikupite hii: Ukiona kifaa kama hiki ondoka mahali hapo haraka sana.

5: Kwa tathmini ya sasa nauli ya Treni hizi haitokuwa sawa na Treni za mita kwani ni Treni zinazotumia teknolojia kubwa na za kisasa, hivyo nauli itakuwa juu zaidi ya Treni za kawaida.

6: Treni haitosimama kama umeme kutoka Tanesco ukikatika ghafla.

7: Kiwango cha nauli kwa wanafunzi bado kinafanyiwa kazi.


8: Kwa sasa watu binafsi hawataruhusiwa kuwa na Treni binafsi kwani Shirika la Reli ndilo litakuwa msimamizi mkuu.