August 19, 2017

Historia fupi ya maisha ya Rebecca Malope.

Rebecca Malope alizaliwa tarehe 30/6/1968, Kanyamazane, South Africa. Mbali na uimbaji Rebecca Malope pia ni host wa Tv Show itwayo "It's Gospel Time".

Safari ya uimbaji wa Rebecca Malope ilianza mwaka 1986. Akiwa na ndoto za kuwa moja kati ya mastar wakubwa huko South Africa na kuwa muimbaji bora zaidi. Katika umri wa miaka 18 Rebecca na dada yake "Cynthia", waliondoka nyumbani kwao kuelekea Evaton (umbali zaidi ya 400 km) kutafuta kazi kwa sababu familia yao ilikuwa maskini na kisha kuelekea Johannesburg.

Mpaka mwaka 2014 Rebecca Malope alikuwa na Album 32. Album yake ya kwanza "Ma g man" aliachia mwaka 1986, Album ya pili "Six of the bestmwaka 1989, na album yake ya tatu "Saturday Nite" mwaka 1990. 

Soma: Historia Fupi Ya Maisha Ya Rose Muhando.

Mwaka 1990, Rebecca Malope alishinda tuzo ya OKTV kama msanii bora wa kike South Africa. Mwaka 1993 zaidi ya watu Million moja walimpigia kura Rebecca Malope katika tuzo za "Cocacola Full Blast Music Awards Music Show" kama msanii anae julikana sana South Africa, Rebecca Malope alishinda tuzo hizo mara mbili, mwaka 1993 na 1994

Mwaka 1995 aliachia album ya 8 "Shwele Baba" na aliuza zaidi ya nakala Million 1 ndani ya wiki tatu, baada ya kuachia album hiyo ya 8, akawa msanii anaeongoza kwa kuuza nakala nyingi ndani ya mda mfupi katika hostoria ya South Africa.

Itaendelea...............