August 2, 2017

Hivi ndivyo shetani alivyoyatesa maisha yangu - Kevin Zakaria.

Bwana Yesu asifiwe sana naitwa Kevin Zakaria nina miaka 20 kabila langu Msukuma ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia yenye watoto (5) na mimi nikiwa ni mtoto pekee wa kiume, nilianza elimu ya (vidudu) mwaka 1999 katika shule moja iliyoko wilayani Urambo mkoani Tabora.

Ilupofika mwaka 2000 nilianza rasmi elimu ya msingi, Baba yangu na Mama yangu wote ni Wasukuma walifunga ndoa mwaka 1990, na mwaka 1991 walifanikiwa kumpata mtoto wao wa kwanza ambaye ni Dada yangu wakiwa kwa wakati huo baba yangu alikuwa kikazi Dar Es Salaam.

Lakini baadae alihamia mjini kahama na mwaka 1994 nikazaliwa mimi Kevin Zakaria, mjini kahama hatukukaa sana, Baba akahamishwa tena na kupelekwa mjini Urambo huko akawa muhasibu wa tumbaku katika kampuni ya (tobaco).

Kiukweli tulipokuwa tukiishi Urambo maisha yalitunyookea, Baba na Mama walifanikiwa kufungua vitega uchumi vingi xana ikiwemo Restaurant, Hotel n.k 
 
Maisha yalikuwa ni ya amani na furaha sana mpaka kufikia mwaka 2001, Baba na Mama walikuwa na watoto (5) na watoto wa mwisho ambao ni mapacha mama aliwapata mwaka huo wa 2001 na yule niliyemwachia ziwa alizaliwa 1996.

katika maisha yetu hayo imani ilikuwa imesimamia katika misingi ya Roman Catholic tukiwa hapo Roman wazazi wangu walifanikiwa kutupeleka kwa Paroko tukabatizwa na kila ubatizo wa mmoja wetu ilikuwa inafanyika sherehe kubwa sana na tulikuwa tunawaalika mapadre na kitu ambacho sitasahau katika sherehe hizo ni kuwaona mapadre wakinywa pombe na wakati huo nilukuwa darasa la (3) kwa hiyo hata mimi sikusita kunywa pombe.

Nimeanza kunywa pombe nikiwa na miaka 8, pamoja na maisha hayo ya kiimani lakini pia baba na mama walitujenga katika misingi ya mila na desturi, kuna wakati baba alikuwa akileta waganaga nyumbani wanatuchanja chale wanachinja mbuzi na kufanya matambiko.

Kiukweli sikuwa naelewa kwa sababu nilikuwa mdogo lakini nilijiuliza sana kwa sababu tulikuwa tukienda kanisa, sanday school ya kiroma tulikuwa tukiambia uchawi ni mbaya sana, binafsi nilikuwa nashangaa sana baba kuleta wachawi nyumbani, na sikuwa na ujanja wowote kwa sababu nilikuwa mdogo chini ya uongozi.

Maisha yalisonga kwa dizain hiyo nilipofikisha umri wa miaka (9) nilianza kijichanganya disko, mwaka 2001 nilikuwa naiba hela ndani kisha najichanganya na kwa miaka hiyo pesa ilikuwa na thamani sana kwa sababu nilikuwa naiba 2000 tu lakini matanuzi yake ni balaa.

Kiingilio disco ilikuwa sh 100, sigara ilikuwa sh 20 kwa hiyo nilikuwa nikiingia disco nilikuwa nina uwezo wa kuvuta sigara 7 na pia isitoshe nilikuwa navihonga visichana tunaenda kufanya mchezo mchafu na ukizingatia baba yangu alikuwa tajiri sana. 
 
Yote hayo niliyafanya kwa sababu ya misingi mibaya ya malezi ya wazazi "Zaburi 11:3". Kuna nyakati ambazo baba alikuwa anarudi home akiwa amelewa na akirudi humo ndani hakukaliki, kingine kilichonifanya nianze ujinga huo mapema ni Tv nilikuwa nikiwaona wanamziki wanafanya hivyo na mimi pia nikaanza kuiga.

Kwa hiyo hayo ndiyo yakawa maisha yangu kwa kipindi hicho na kama unavyojua gari ikibadili gia spidi inaongezeka, basi ikafika kipindi nikawa naenda kwenye hotel ya baba na kuanza...!
                 
....Usikose seheme ya pili ya ushuhuda wangu....