August 1, 2017

Jinsi ya kupika chapati.

Vipimo
Unga wa ngano mweupe ................... 1 Kilo
Samli .............................................. 150gm
Chumvi ............................................3 vya chai
Maji ya moto yasichemke lakini ........... Kiasi
Mafuta Ya Zaituni (olive oil) ................ 4 vijiko vya supu
Samli tena ....................................... 200 gms
Iliki iliyosagwa ...................................1 kijiko cha chai


Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Tia unga kwenye sinia au bakuli kubwa lilo na nafasi, changanya na chumvi, mafuta ya zaituni, samli 150g, iliki, mimina maji ya moto kwa kipimo cha kikombe kila unapovuruga unga.

2. Unga uwe mwepesi unapoganda kuwa donge moja kubwa. Uwache kwa muda wa dakika 20 – 30 ukiwa umeufinika ili unga ulainike.

3. Katakata madonge makubwa yenye ukubwa wa chungwa ili uweze kutoa kila donge chapati mbili. Ukimaliza hapa weka madonge kwa muda wa dakika 15 ukiwa umefinika bila ya kuingia upepo ndani.
4. Sukuma donge ukiwa umelimwagia unga mkavu juu, liwe mviringo. Unaweza kutumia kifimbo hata chupa kusukumia madonge ikiwa huna kifimbo juu ya meza au kwenye kibao maalumu cha chapati.

5. Sukuma donge moja mpaka liwe duwara jembamba.

6. Paka samli kama kijiko kimoja cha kulia, ukihakikisha umepaka duwara lote.

7. Kunja lile duwara kama mfano wa kamba, huku unazungusha kama kamba ili iwe ndefu kidogo.

8. Zungusha ile kamba iwe mviringo. Funika na kitambaa kisafi cha jikoni ambacho kimajimaji kidogo.

9. Endelea namna hii mpaka umalize madonge yote.

10. Sukuma chapati iwe mviringo kama nchi 7 hivi.

11. Weka chuma cha kuchomea chapati jikoni moto mdogomdogo.

Pika chapati kwenye frying pan, moto uwe wa kiasi. Ikiiva upande mmoja na kuanza kufura, geuza upande wa pili. Tumia kitambaa kisafi cha jikoni kupress na kuzungusha zungusha ile chapati. Ikiiva upande wa pili, mimina kijiko kimoja cha chakula cha samli na ugeuze chapati tena, zungusha zungusha kisha mimina nusu kijiko cha kulia cha samli na ugeuze upande wa pili kidogo. Toa chapati uweke kwenye sahani. Ikunje kunje kidogo kisha uifingue vizuri.

Zipange kwenye sahani huku unazifinika, hapa tayari kuliwa kwa mchuzi au mboga yoyote.