August 10, 2017

Jinsi ya kuthibitisha kama mtu anakupenda kwa dhati.

Ukweli ni kwamba, Hakuna njia kuu ya kukuwezesha kuthibitisha moja kwa moja kama mtu anakupenda, lakini zipo ishara chache za kitabia zitakazoweza kukusaidia kutambua kilichopo katika mawazo ya mpendwa wako. 


Ukitaka kujua kama unapendwa na mtu unayempenda zitazame tabia zake juu yako. Ingawa upendo una mana tofauti kwa kila mmoja wetu, zipo njia nyingi zinazoweza kukueleza kama kweli mtu anakupenda kwa dhati, Tena zinazoweza kukupa tofauti ikiwa kama mtu anakupenda kwa dhati au amekutamani tu!

ANGALIA ANAVYOFANYA.

1. ANGALIA KAMA ANAWEZA KUTENDA MAMBO KIKAWAIDA UNAPOKUWA NAYE.
Moja ya sehemu muhimu katika mapenzi ni kuwa muwazi kwa Yule umpendae. Kama unapokuwa naye umeanza kuona baadhi ya tabia au mambo fulani ambayo huwa hayaoneshi hadharani, ujue kapenda huyo! Kwa mfano, kama mpenzi wako huwa ni mpole na mtaratibu sana anapokuwa na umma, lakini mnapokuwa peke yenu anakuonesha mbwebwe na utani wake mwingi, mambo ambayo hawezi kuyafanya hadharani, ujue wazi anafunguka kwako na ni ishara kuwa anakupenda kwa dhati.

Kama mtu anakushirikisha hisia zake kikamilifu na anajisikia huru kufanya hivyo, huo ni upendo!!!
Kama mtu anajisikia huru kutokuwa mkamilifu mbele yako, mfano; hajisikii vibaya ikiwa utabahatika kukiona chakula kimemkwama katikati ya meno yake la mbele, au kukohoa (kubanja) mbele yako, yupo huru kukushirikisha pande zote za maisha yake kwasababu anakupenda kwa dhati.


2. CHUNGUZA UONE KAMA HUWA NI MWENYE FURAHA ANAPOKUWA KARIBU YAKO.
Inapaswa kuwa hivyo hata katika siku yenye changamoto kwake. Kama mpenzi wako alikuwa na siku yenye changamoto au siku mbaya kama wengine waiitavyo lakini unamuone mudi yake inabadirika na kuwa yenye furaha mara tu anapokuona, basi hiyo ni ishara ya upendo kwako. Kama kweli anaugulia penzi lako, sura au sauti yako vinatosha kumpa faraja na kuivuta furaha maishani mwake – hata kidogo.
  • Siku nyingine mpenzi wako akiwa na siku mbaya, pima uone anavyoichukulia kampani yako licha ya kuwa na changamoto zake binafsi.


3. JE, ANAKUTUPIA JICHO LA SHAUKU KUBWA?
Ingawa inaweza kuonekana kama kwamba ni uchizi, lakini nakushauri siku nyingine ukikutana na mpenzi wako, utazame uso wake na kisha uone kama anakutazama kwa shauku kubwa. Utajua tu ukimtazama kwasababu huwa hali hiyo haionekani mara zote! Unaweza kupata mwanya huo wakati wa asubuhi au muda wowote hasa wakati wa chakula cha mchana mkiwa mezani.
  • Unaweza pia kumkamata akiwa anakukodolea macho kwa shauku kubwa vilevile.