Featured Posts

August 10, 2017

Jinsi ya kuthibitisha kama mtu anakupenda kwa dhati. (Part 3)

5. TARAJIA KUKUMBUKWA HASA UNAPOKUWA MBALI NAYE.
Kama mtu wako anakukumbuka kwa kukutumia ujumbe wa maneno kupitia simu yake, kukupigia simu, kukutumia barua pepe, kuchat na wewe mara kwa mara unapokuwa mbali naye hali akijaribu kukueleza jinsi alivyo kukumbuka, hiyo inamaanisha nini? – Anakuonesha ni kwa jinsi gani hawezi kuyaendesha maisha yake bila ya wewe.  Kama ukiona umekaa mbali na mtu wako kisha unaona ukimya tu! ndio unashamiri jua wazi hakuna mapenzi hapo.

 • Sio lazima akupigie simu mfurulizo akueleze kuwa amekumiss ndio ujue kuwa anakupenda. Kumbuka kuwa ana majukumu pia, hivyo kama na wewe unampenda zingatia uwiano wa mapenzi yenu na kazi.

6. TARAJIA KUKOSOLEWA PINDI UNAPOKOSEA.
Kama kweli mtu wako anakupenda, ninaamini hawezi kuitunza picha yako ya kughushi kichwani mwake. Mtu anayekupenda kwa dhati daima atajijitahidi kukurekebisha na pia kukukosoa kwa busara pindi unapokosea. Hiyo ni ishara kuwa anakupenda jinsi ulivyo na pia anakubali mapungufu yako lakini anapenda uwe bora zaidi. Ingawa hatakiwi kukukosoa muda wote vilevile anayekupenda hawezi kukukosoa mbele ya watu kwakuwa anakuheshimu.

 • Kama mtu wako hajawahi kukukosoa au hata kukwaruzana na wewe kidogo, nakushari utafute mlango wa kutokea kwasababu hakuna mwanadamu anayeuweza wa kutenda kwa usahihi asilimia mia moja. Anayekupenda hatoyafuga makosa yako kwa kuitunza picha yako feki kichwanii mwake.

7. ANGALIA KAMA ANAHESHIMU FIKRA ZAKO.
Kama kweli mtu anakupenda daima ataziheshimu fikra zako. Haijarishi ni ushauri juu ya mavazi au matatizo yake binafsi daima atahehimu ushauri wako, atafanya hivyo kwasababu anakupenda na hivyo anataka utambue uthamani wako kwake.

 • Kumbuka kwamba sio lazima aombe ushauri katika kila kitu – atafanya hivyo hasa kwa yale mambo muhimu.
TAZAMA MATENDO YAKE.

1. TARAJIA KUSIKILIZWA.
Kama kweli mtu anakupenda kwa dhati, hawezi kuishia kuwa muwazi kwako bali atakusikiliza pia. Hata kama amewahi kuyasikia maneno hayo kabla lakini kama anakupenda atakutegea sikio tena na tena kwasababu anahesimu fikra zako. Ingawa hatokuwa kama mbwa wako lakini atajitahidi kwa kadri awezavyo kukutegea sikio.

 • Moja ya mambo muhimu unayopaswa kujifunza kabla na baada ya kuingi katika mapenzi ni usikivu, na si kuishia kuongea tu! – Kama unavyopenda kusema na mwingine asikilize, vilevile uwe tayari kukaa kimya na kusikiliza maoni, maonyo na mafundisho ya mpenzi wako pia.

2. ANGALIA KAMA YUPO KWAAJILI YAKO.
Hii inajumuisha nyakati nzuri na mbaya pia. Je, unapokuwa na huzuni na unahitaji faraja ya ukaribu au Unapokuwa mgonjwa, yupo tayari kutenga muda wake kwaajili yako? Na Vipi unapohitaji Kampani yake kutoka Out kupata chakula au kinywaji au unapohitaji kusikia sauti yake usiku wa manane, yupo tayari kuyaweka mambo mengine kando angalau hata kwa nusu saa kwaajili yako?

 • Kama mtu anajumuika na wewe nyakati unapokuwa na furaha tu na kisha kukutenga anapogundua una huzuni au unaumwa, huo sio upendo yupo hapo kutafuta kukidhi haja ya mwili wake na sio kutafuta penzi la milele.
 • Mapenzi maana yake kuwepo kwajili ya mwenzi wako, bila kujali chochote. Na upendo wa kweli maana yake ni kumkubali mtu katika mapungufu na mazuri yake bila kuchokan na kuwa naye katika nyakati nzuri na mbaya pia.

3. ANGALIA MAMBO MAZURI ANAYOKUTENDEA.
Mtu anayekupenda kwa dhati atajitahidi kukutendea mambo mazuri kwa kadri awezavyo, kukufundisha mambo usiyoyajua, kukutembelea na kukuletea zawadi uwapo mzima au mgonjwa, kukupikia, kukufulia nguo au kukuoshea vyombo na mambo mengine mazuri ya siyo na kikomo, atafanya hayo yote  kwasababu wewe ni furaha yake na hivyo hawezi kuiruhisu siku ipite pasipo kuiona furaha ikishamiri maishani mwako.

 • Mapenzi ya dhati hayaishii katika kile unachochukua kutoka kwa mtu bali kile unachoweza kukitoa pia kwaajili yake.
 • Mtu anayekupenda hatosubiri kuombwa ndio akutendee mambo mazuri.

4. ANGALIA KAMA ANAPENDA KUWEPO KARIBU YAKO.
Moja ya raha kubwa katika mapenzi ni ile hali ya kutaka kuwa karibu na Yule umpendaye nyakati zote. Mtu anayekupenda atajitahidi kuwa karibu yako kwa kadri awezavyo. Haina maana kuwa atakuganda kama luba, bali atajitahidi kuwa na wewe mara nyingi awezavyo na kwa kadri ya nafasi yake.

5. JE, ANAKUPA UHURU?
Kama kweli mtu  anakupenda kwa dhati atajitahidi kukupatia uhuru wa kufanya mambo yako mwenyewe bila hata kuambiwa au kuombwa. Kama watu wazima na mlio starabika mtatambua kuwa mnahitaji kupeana uhuru wa kufanya mambo yenu binafsi kutunza heshima yenu mbele ya jamii zinazowazunguka.

 • Kama unaona mtu wako anakuganda kuwa nawe muda wote ni darili ya kuwa hakuamini kama unaweza kusimama mwenyewe bila yeye kuwepo karibu yako, jambo ambalo haliashirii upendo kwasababu kuaminiana ni sehemu ya upendo wa kweli.

6. ANGALIA KAMA ANAKUELEWA.
Upendo wa kweli ni maelewano thabiti. Mpendwa wako anapaswa kukuelewa ili akupende zaidi, kutambua anachokitaka, unachokipenda na unachokichukia, mambo yanayokupa furaha, hata mabadiliko yako kihisia kwani kwa kufanya hivyo itampa wepesi wa kukupenda pasipo hali ya kudhani.

 • Simanishi kuwa mtu wako anapaswa kukuelewa asilimia 100%, najaribu kukupa mwangaza kuwa utambue kama anatambua hisia zako, unayoyapenda na unayayoyachukia? Na je, anaweza kukufurahisha?

7. ANGALIA KAMA ANAKUTAKIA MEMA.
Hapa najumuisha hata yale mambo ambayo hayana faida kwake. Kama mtu anakupenda kwa dhati atakuwa mwelewa hata unapotakiwa kuwa mbali nay eye kwa kipindi cha muda Fulani ili uweze kufanikisha mamo yako, kwa mfano kama ni wewe ni mwanafunzi ataktakiwa kuelewa kwamba kuna kipindi utamuacha na kuelekea mikoa au hata nchi za nje kwaajili ya kukamilisha masomo yako, au kama wewe ni rubani, nahodha au dereva wa magari ya masafa malefu atatakiwa kutambua kuwa inakupasa ukae mbali naye kwa siku kadhaa ili utafute pesa badala ya kushinda tu mitaani.

 • Nina maana kwamba kama mtu anakupenda kwa dhati atajiongeza kwa fikra chanya juu ya majukumu yako kuwa yana faida kwenu wote na si kwako peke yako.

8. ANGALIA KAMA NI MSAADA KWAKO.
Kama kweli anakupenda hatoishia kuwepo tu karibu yako bali atakusaidia katika shughuli zako ili ufanikishe ndoto zako na usonge mbele. Kama anakupenda atakusaidia kuandaa mpango wa biashara na mtaji pia ikiwa ana uwezo, atakusaidia kimasomo, atakusaidia kukuandaa na interview ya ajira, atakufundisha kupanga bajeti yako, atashiriki na wewe wajibu mbalimbali za kiroho na mambo mengine zaidi. Kwa ufupi ni kwamba atakuwepo kusikiliza jambo lolote linalokutatiza – kwaajili yako.
 • Kama anakupenda atakusaidia kufanikisha malengo yake hata kama katika namna moja au nyingine hayana faida kubwa kwake.