August 2, 2017

Historia fupi ya maisha ya Millard Ayo (Part 2).

Alifanikiwa kupata kazi May 23 2005 kwenye kituo cha Wapo Radio 98.0 ambayo aliambiwa hatolipwa kwa sababu kanisa lililokua linamiliki radio hiyo halina pesa ila kwa sababu alikua na njaa ya maisha na kazi ilibidi aifanye kama ameajiriwa, kazi ilikua jumatatu mpaka jumamosi kuanzia saa mbili asubuhi huku kazi yake kubwa aliyopangiwa ni kukusanya habari za bei za bidhaa na hali ya usafi kwenye masoko Dar es salaam, pia kwenda kitengo cha MOI Muhimbili hospitali kuchukua habari za majeruhi na vifo vya ajali mbalimbali.

Isikupite hii: Mambo 10 usiyojua kuhusu Vatican.


Kutokana na jitihada hizo Millard alianza kulipwa shilingi elfu tano kwa wiki mwezi wa pili baada ya kazi hivyo akawa na mshahara wa elfu 20 kwa mwezi, mshahara ambao uliongezeka na kufikia elfu 20 kwa mwezi kwenye mwaka wa tatu na wa mwisho akiwa Wapo Radio.

Baada ya hapo Millard alijiunga na ITV/Radio One mwaka 2008 ambako alisikika kwenye vipindi mbalimbali lakini MILAZO 101 na habari za michezo ITV ndio vilimpa umaarufu mpaka November 2010 alipojiunga na Clouds FM/TV na kuanza kusikika kwenye kipindi cha AMPLIFAYA december 6 2010 na baadae kukabidhiwa CLOUDS FM Top 20 June 2013.

Mpaka sasa Millard Ayo ni mmiliki wa tuzo 4 ikiwemo ya Mtangazaji bora 2006 kutoka Tanzania Radio Awards, Website bora 2012 kutoka Vodacom Tanzania na African Stars, na moja ni ya heshima akiwa mwandishi pekee kutunukiwa kutoka kwenye familia ya Marehemu mwigizaji Steven Kanumba.

Kipindi cha AMPLIFAYA pamoja na website yake ya millardayo.com ndio vilivyofanya ukubwa wa jina lake uongezeke.

Isikupite hii: Fahamu faida za pweza kwenye afya ya mwanadamu.

Kitu ambacho watu wengi hawakifahamu, kipaji cha Millard Ayo kilionekana kwanza na aliyekua mtangazaji wa TBC1 Joseph Msami ambae kwa wakati huo ndio aliona uwezo wa Millard na kumshawishi boss wa Wapo radio kutoa ruhusa ya Millard kuingizwa studio kuwa mtangazaji na sio tena ripota.