August 2, 2017

Historia fupi ya maisha ya Millard Ayo (Part 3).

Mtu wa pili ambae ndio alizidi kumnyanyua Millard kiutangazaji ni Godwin Gondwe ambae alimuona Millard toka akiwa Wapo Radio, kwanza ndio alikua mtu wa kwanza kumpa Millard dili la kurekodi tangazo la radio la bei kubwa 2007 toka ameanza utangazaji, lilikua la laki moja na nusu za Kitanzania na ndio ilikua pesa kubwa Millard kuwahi kulipwa kwa kazi ya mikono yake toka azaliwe, na ni pesa kubwa kuliko hata mshahara wake kwa mwezi wakati huo ambao ulikua shilingi elfu sitini.

Isikupite hii: Tabia 8 za watu wapole - Dr. Chris Mauki.

Shukrani za pekee kwa Reginald Mengi, Joyce Muhavile, Julius Nyaisanga, Deogratius Rweyunga, Abdallah Mwaipaya na Isack Gamba ambao walikua kama wazazi/marafiki wakati Millard akiwa ITV, pamoja na kwamba kwa sasa hayupo ITV lakini urafiki wao haujaisha na Millard amekua balozi wao mzuri

Watu wengine waliomfikisha Millard hapa alipo kwa kiasi kikubwa ni Gardner G Habash ambae wakati Millard akiwa Wapo Radio alimsaidia sana kumpa nafasi ya kusikilizwa Clouds FM ambako alipata kazi ya kuanza na kipindi cha gospel lakini wiki hiyohiyo ndio akaitwa ITV, Reuben Ndege nae alicheza kwenye uwanja mkubwa zaidi kumsuka Millard Ayo alipojiunga na Clouds FM na alijaribu sana kumshawishi Millard kujiunga nao wakati akiwa Radio One, kiukweli siku zote amekua msaada mkubwa wakati wote na supporter mkubwa kwa Millard.

Sebastian Maganga ambae ni mkuu wa vipindi Clouds FM amekua msaada mkubwa sana kwa Millard Ayo, mshauri na hata ndugu ambae ni msikilizaji mzuri sana pale Millard anapozungumza nae na ndio alipendekeza Millard kuchukuliwa Radio One wakati huo.

Ruge Mutahaba amekua boss, kaka, mshkaji na mshauri wakati wote kwa Millard Ayo, kwa kiasi kikubwa pamoja na kwamba alitoa idhini ya Millard kujiunga na familia aliyokua anaipenda kwa zaidi ya miaka 10, amekua ni msaada mkubwa sana kwa Millard, kuna vitu vingi Millard alikua anasema hawezi lakini Ruge amempa neno na kumpa nguvu kwamba anaweza na ndio mafanikio ya Millard yameanza kuonekana hapo.

Isikupite hii: Aina 5 ya watu ambao hawafanikiwi katika maisha.

Big Boss Joseph Kusaga ambae ndio MD wa Clouds FM, nae amekua mshkaji, boss na kaka kwa Millard Ayo, nguvu ya neno lake kwamba ‘i’am proud of you’ pekee ndio linampa Millard Ayo nguvu kubwa ya kujituma zaidi na kutumia saa kadhaa kuandaa vipindi vyake siku zote na kujituma zaidi