August 12, 2017

Madhara ya vipodozi kwa wamama wajawazito.

Utumiaji wa Vipodozi, ambavyo vina kemikali huchangia ongezeko la wanawake ambao wanatarajia kujifungua wakajifungua watoto kwa njia ya upasuaji.

Wanawake wengi wamekuwa na tabia ya kwenda kwenda maduka ya vipodozi ili kuweza kupata vipodozi hivyo ambayo kwa ueredi Serikali Kupitia TFDA wamekuwa kwenye vita ya kupinga matumizi ya vipodozi hivyo na kutoa onyo kwa watumiaji na wauzaji.

Isikupite hii: Magonjwa 10 muhimu ya kupima na mpenzi wako kabla ya kuzaa mtoto.

Watalamu, wa afya, wamedadavua, kuhusiana na madhara ya vipodozi venye kemikali, ikiwemo lotion, sabuni ambazo zinakuwa na kemikali kama Mercury, Hydroquinone na Steroids, kwa mujibu wa wataalamu wa afya, wasichana na wanawake watapata madhara badae, Aidha, tafiti hiyo inaonesha kuwa watumiaji, wa vipodozi, hivyo wapo kwenye hatari,ya kupata magonjwa ya ngozi, na kuumwa Ugomjwa wa Ini kutokana na kemilkali ambazo zimepenya ndani ya Mwili pale unapotumia madawa ya kubadilisha ngozi ambayo yanapatikana katika losheni na cream na sabuni zina kemikali ambazo sio rafiki.

Pia, Wakati wa kujifungua wanawake au wasichana walio athirika na vipodozi hivi vya kujichubua wanapata tabu kwenye kipindi cha kumsumkuma mtoto kwani ngozi, inakuwa haina uwezo wa kuhimili ukakamavu wakati wa kujifungua na kusababisha kupasuka kwa mfuko wa uzazi na kupelekea kufanyiwa operation ili kuokoa maisha ya mama na mtoto, Vilevile, kuna uwezekano wa kupoteza ujauzito (miscarriage), hali hii inasababishwa na kemikali ambazo zinapatikana kwenye vipodozi kuwa na atahri kwenye mfuko wa uzazi na kusababishia udhaifu wa kuwa laini  na kushindw kubeba kijusi au mtoto aliyetumboni.

Isikupite hii: Tambua vyazo 10 vya kuharibika kwa mimba

Wataalamu hao, wamesema kuwa kemikali hizo, husababisha madhara kwa mtoto aliyetumboni kwa kumfanya awe na matatizo mbalimbali ya kiafya pale anapozaliwa.

Pamoja na Serikali kuwa na njia yakinifu kupitia TFDA, ya kudhibiti matumizi ya vipodozi vyenye kemikalilakini bado Watumiaji wanazidi kuitupa gizani nguvu ya serikali ya kuwaepusha na madhara yatokanayo na matumizi hasi ya vipodozi vyenye kemikali.