August 6, 2017

Mtoto akutwa na sindano 7 mwili zilizoingizwa kichawi - Maajabu.

Mtandao maarufu wa Daily Mail  July 28, 2017 uliripoti kuwa mtoto wa kike aliyekuwa na umri wa miaka mitatu amefariki baada ya kutumiwa kichawi na boss wa mama yake ikiwemo kunyanyaswa kijinsia.

Mtoto huyo aliwahishwa Hospitalini katika mji wa Kolkata, Magharibi ya Bengal akiwa katika hali mbaya ambako baada ya kufanyiwa uchunguzi aligunduliwa kuwa na sindano saba katika mwili wake zilizoingizwa kishirikina.

Isikupite hii: Kutana na Ramesh Babu kinyozi anayemiliki magari 75. (+video)

Taarifa ya Polisi inasema kwamba mtu anayeitwa Sanatan Thakur, ambaye hujihusisha na masuala ya nguvu za giza alimuajiri mama wa mtoto huyo kumfanyia kazi za ndani na kumtumia mtoto huyo katika mambo ya kishirikina.

Ingawa Madaktari walifanikiwa kuziondoa sindano zote saba, mtoto huyo alifariki.