August 1, 2017

Mwanangu nisikilize mimi, hii ni kwa wanaume wote.

1. Mwanangu ninaposema wewe utakuwa kichwa cha nyumba katika ndoa yako, simaanishi uwezo wako wa kipesa na kutunza familia. Bali ni kuhakikisha kila siku tabasamu la mkeo halitoweki. 

2. Mwanangu, usijisahau pale utakapofanikiwa kutengeneza pesa, badala ya kutumia hizo pesa na wanawake vicheche ambao hawajui ni jinsi gani ulivyozihangaikia, ni bora ukatumia na mwanamke ambae alisimama bega kwa bega na wewe mpaka ukawa nazo. 

3. Mwanangu kumbuka, pale utakaposema mke wangu amebadilika, basi ujue kuna kitu wewe umesitisha kumfanyia. 

4. Mwanangu mama yako aliendesha baiskeli na mimi kabla sijapata visenti vya kununulia motokaa. Mwanamke yeyote ambae hatakuwa na weww wakati wa shida kamwe asifurahie matunda uliyovuna. 

5. Mwanangu, usimfananishe mkeo na wanawake wengine, kuna mambo ambayo na yeye anakuvumilia tu! Kwani ashawahi kukufananisha na wanaume wengine? 

Isikupite hii: Faida 10 za mayai ya kuchemsha.

6. Mwanangu, sikuwapeleka dada zako shule kwa sababu nilikuwa mpumbavu kwa kufikiri kusomesha watoto wa kike ni hasara. Tafadhali sana nawe usifanye kosa hilo. Mafanikio nayoyaona hivi sasa kwa wanawake yamewafanya wawe wa muhimu sana. Wasomeshe watoto wote kwa usawa. 

7. Mwanangu, mimi na mama yako hatuko interested na kike kitakachokua kikitokea katika ndoa yenu, jaribuni kusuruhisha mambo yenu wenyewe pasina kuja kwetu. 

8. Mwanangu, kumbuka nilimnunulia mama yako cherehani yake ya kwanza. Msaidie mkeo azifikie ndoto zake kama jinsi wewe unavyojitahidi kufikia malengo yako. 

La muhimu mwanangu, Omba Mungu na familia yako, kuna kesho ambayo hauijui. Ongea na Mungu kwa sala kwani yeye ndiye ajuaye kesho zetu.... Nakupenda Mwanangu, enenda ukawe Mume Bora, kamwe usiniangushe.