August 5, 2017

Vitu vya kuzingatia wakati wa kujenga msingi wa nyumba yako.

VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUJENGA MSINGI WA NYUMBA YAKO
Kuna aina mbalimbali za msingi na ili kuweza kuchagua msingi wa nyumba kunategemea vitu vingi sana, moja wapo ni aina ya udongo uliopo kwenye site yako. Nyumba ambazo zinajengwa kwenye udongo dhaifu huitaji msingi wenye kina.

Hali ya hewa pia ni kitu cha muhimu kuzingatiwa, aina nyingine za msingi hushindwa kua imara sehemu zenye unyevu mwingi au baridi kali.


Isikupite hii: Zingatia vifuatavyo kabla ya kununua kiwanja. 

Aina ya nyumba unayotaka kujenga pia itategemeana na msingi. kama ni Ghorofa basi msingi uwe imara wa kuweza kubeba uzito wa ghorofa hilo.

Ni vizuri kushauriana na wataalam wakati unataka kuweka msingi ili wakushauri ni aina gani au kiwango gani cha msingi kinachohitajika.