Featured Posts

August 7, 2017

Watu wenye vinyweleo vingi mwilini waweza kuwa na akili nyingi?

Dr. Aikarakudy Alias ambaye ni daktari wa magonjwa ya akili, ambaye amekuwa akichunguza kwa miaka 22 uhusiano kati ya vinyweleo katika mwili na uwezo wa akili, aliwaambia wanachama wa chama cha European Psychiatrists katika mkutano wao kuwa, vinyweleo vingi hupatikana kwa wingi hasa kwa madaktari na watu wengine waliosoma sana katika jamii kwa ujumla.

Uchunguzi wake ulifanywa miongoni mwa wanafunzi wanaosoma udaktari nchini Marekani na aligundua kuwa asilimia 45 ya wanafunzi walikuwa na vinyweleo hasa katika vifua vyao Ukilinganisha na asilimia 10 ya watu wenye elimu ya kawaida ambao hawakuwa navyo au walikuwa navyo kwa uchache.

Katika mji wa Kerala, kusini mwa India, uchunguzi miongoni mwa wanafunzi wa udaktari na uhandisi ulionesha kuwa makundi yote wana vinyweleo vingi ukilinganisha na wale wanafanya kozi za kawaida.

Pia matokeo yalipotoka yalionesha kuwa wanafunzi nane wa kwanza walikuwa na i kwaniviyweleo vingi kuliko wanafunzi nane wa mwisho.

Alihitimisha kuwa wanaume wenye vinyweleo vingi huwa na akili nyingi ingawa pia wapo wasio na vinyweleo vingi wenye akili nyingi kwani hata Albert Einstein hakuwa na vinyweleo.