August 2, 2017

Tazama picha za mtu mrefu na mfupi zaidi duniani walipokutana kwa mara ya kwanza.

Tumekuwa tukisikia rekodi mbalimbali zikivunjwa na watu duniani na rekodi hizo maalumu huwa zinatunzwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Guiness World Records.

Kwa mara ya kwanza, watu ambao wako katika kitabu hicho kutokana na kuvunja rekodi hizo za kipekee wamekutana London Uingereza siku ya Novemba 13.

Chandra Bahadur Dangi mtu aliyevunja rekodi ya kuwa mtu mfupi kuliko wote Duniani amekutana kwa mara ya kwanza na Sultan Kosen, jamaa ambaye amevunja rekodi ya kuwa mtu mrefu zaidi duniani.

Chandra anatokea Nepal ana urefu cha Sm. 54.6, Sultan anatokea Uturuki ana urefu wa Sm. 251 ambayo ni sawa na futi 8.3.

Hizi ni picha zinazowaonyesha wakali hao wakiwa pamoja.