August 8, 2017

Shetani atukuzwa na kutunukiwa sanamu nchini Marekani .

Katika hali isiyo ya kawaida na ile inayoashiria kwamba mwisho wa dunia u karibu, dunia imeshuhudia mamia ya wakazi wa Detroit nchini Marekani wakijipanga msururu kushangilia kuzinduliwa kwa sanamu siku ya Jumamosi tarehe 25 Julai 2015, yenye kumtunuku ukuu.

Sanamu hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya shaba lenye uzito wa tani moja na urefu wa futi tisa, ina umbo la mtu, kichwa cha mbuzi, na mabawa, huku miguu yake ikiwa na kwato, na huku kando yake watoto wawili wakiwa wanamtazama.

Taharuki kuhusu sanamu hiyo ilianza wiki kadhaa nyuma, ambapo watengenezaji walitaka kuisimika kando ya mnara wenye amri kumi za Mungu kwenye mji wa Oklahoma. Hata hivyo juhudi za mashabiki hao wa shetani hazikufua dafu baada ya kupata pingamizi kutoka makundi mbalimbali ikiwemo waamini mbalimbali na wazazi.

Jambo hilo halikuwasumbua wapenzi hao wa kiongozi mbaya duniani, ambapo waliamua kuahirisha uzinduzi wao na kupanga ratiba zao kimya kimya ili wapate kufanya kwa surprise, na hatimaye usiku wa saa tano na nusu, mamia ya watu wakajongea eneo la tukio na kadi zao zia mialiko ili kuwa mashuhuda wa tukio hilo la kihistoria la kipekee kwao, ambapo ikazinduliwa na kwa wanaume wawili kuondoa kitambaa ambacho sanamu lilikuwa limefunikwa, na kisha baada ya hapo kubusiana mbele ya sanamu hilo, huku kelele za furaha zikisikika.


Sanamu katika hatua za awali za matengenezo.
Hata hivyo tukio hilo bado limepata pingamizi miongoni mwa wanajamii, wakiwemo wakristo, ambapo walikuwa na maombi kukataa tukio la kumkabidhi shetani mji wa Detroit. Mchungaji wa kanisa la Greater St Mathew Baptist, Dave Bullock, amesema kwamba jambo kama hilo halikubaliki na kamwe hawataliruhusu. Katika maelezo ya waandaji, wenyewe walitoa mualiko wakisema, "come dance with the devil and experience history in the making", yaani kwamba njoo ucheze na shetani ukishuhudia historia inavyoandikwa. Tukio hilo lilihudhuriwa na watu wenye umri kwanzia miaka 18, na halikuruhusu upigaji wa picha, isipokuwa tu kwa wale VIP, ambao walipata fursa ya kupigwa picha kando ya sanamu hilo na kisha kufanyika utaratibu wa kupata picha zao. 

Baada ya tukio hilo la uzinduzi, picha za tukio ambazo wamezitoa kwenye ukurasa wao wa facebook huku wakiwashukuru washiriki wote, na kuahidi kuachilia picha zote kwa kadri siku zitakavyokuwa zinaenda. Hizi ni baadhi tu, kwani hazifai mbele ya jamii.Je, huu ni mwanzo wa mashabiki na wafuasi wa shetani kujitokeza waziwazi? Mwisho wa dunia umekaribia kwa kiwango gani?