August 10, 2017

Jinsi ya kuthibitisha kama mtu anakupenda kwa dhati. (Part 2)

4. ANGALIA KAMA HUWA ANACHIZIKA UNAPOKUWA KANDO YAKE.
Mapenzi huwafanya watu wajisikie kuchizika, wepesi na wakati mwingine wajisikie kucheka bila sababu yoyote. Kama ukimuona mtu anafanya hivyo unapokuwa kando yake jua kakuzimia huyo!

Isikupite hii: Je unataka upate mtoto wa kiume? Au wa kike? soma hapa

 • Kama ikitokea umeongea jambo ambalo hata si lakuchekesha kivilee alafu unamuona mpenzi wako anafyatuka kwa kicheko kikubwa, jua atakuwa ana homa ya mapenzi juu yako huyo!!!
 • Kama ukimuona mpendwa wako anajisikia na nguvu na furaha ya ajabu kira mara unapokuwa kando yake, ujue hayo ni mapenzi tu yanamuwasha.

5. ANGALIA KAMA HUWA ANAHUZUNIKA PINDI UNAPOKUWA NA HUZUNI.
Kama unaumwa au una uchungu mkubwa moyoni kutokana na changamoto mbalimbali za kimwili au kiroho, si ajabu kumuona mpenzi wako akihuzunika kwa sababu ya hali yako. Kama kweli anakupenda lazima uchungu wako umwingie moyoni mwake pia kwasababu hakuna anachopenda zaidi ya kukuona ukiwa katika furaha yako ya siku zote.

 • Ingawa sio lazima ahuzunike kwa kiasi kikubwa kama wewe lakini ni lazima aguswe katika namna moja au nyingine kwasababu kwa kadri ya upendo wake kwako daima hukutakia furaha tu na si vinginevyo.

ZINGATIA MANENO YAKE.

1. ANGALIA KAMA HUWA ANAYAZUNGUMZIA MAISHA YENU YA BAADAE.
Kama mtu anakupenda, wazo la wewe kuwa ndani ya maisha yake huwa halimtatizi kabisa. Kama mara kwa mara huwa unamsikia mtu wako akizungumzia jinsi maisha yenu yatakavyokuwa baadae miaka miwili au kumi mkiwa pamoja. Kuna uwezekano mkubwa mtu huyo anakupenda kwa dhati na anataka uwe wake siku zote.

 • Kujitoa kweli kwaajili ya mapenzi, maana yake kuamua kuwa naye daima. Kama mtu anapenda kuzungumzia maisha yake ya baadae hali akikujumuisha na wewe ndani yake, hiyo ni ishara tosha ya kuwa mtu huyo anakupenda na anakuhitaji uwepo maishani mwake siku zote za maisha yake.
 • Pia kama mtu wako anapenda kuongelea kuhusu watoto wenu watakavyo kuwa, au mahali mtakapo fanyia “honey-moon” yenu na mambo mengine yanayoendana na hayo, ni ishara kuwa anakupenda na anakuhitaji maishani mwake.


2. ANGALIA KAMA ANAKUPA SIFA ZA MSINGI.
Kuna tofauti kubwa kati ya kauli hizi “Napenda Muundo wa Nywele Zako” na “Unao Uwezo wa Kunifanya Nijisikie Vyema Katika Hali Yoyote Ile” Kama mtu wako anakupa sifa zinazoonesha kuwa anavutiwa na tabia na utu wako, upo uwezekano mkubwa kuwa mtu huyo anakupenda kwakuwa uzuri wa nje huleta mvuto lakini  tabia na utu wako utauteka moyo wa mtu.

 • Sio lazima mpenzi wako akumwagie sifa muda wote – Kumbuka kuwa ni Ubora wa kitu ndio unaozingatiwa hapa na si idadi ya vitu.
 • Kumbuka na zingatia usemi huu – “uzuri wa nje huleta mvuto lakini tabia na utu wako vitauteka moyo wa mtu”

3. TAMBUA KAMA MTU WAKO ANAKUTAMKIA NENO “NAKUPENDA” KWA KUMAANISHA.
Kuna tofauti kubwa kati ya mtu anayekutamkia nakupenda kwa kumaanisha na Yule anayekutamkia neno hilo hilo kwa lengo la kupata kitu fulani kutoka kwako. Ukiona mtu wako anakutamkia neno “Nakupenda” hali akiyatazama macho yako kwa kujiamini. Ni ishara ya kumaamaanisha upendo juu yako.

 • Mtu anayekupenda atakutamkia neno “Nakupenda” mara nyingi bila sababu yoyote, na si kwasababu anahitaji chochote kutoka kwako au anajiskia kuwa ni neno zuri kumtamkia mpenzi wake bali ni kwasababu anatoa kile kilicho ijaa nafsi yake – upendo wake wa dhati kwako.
 • Pia mtu anayekupenda haoni haya kukutamkia “Nakupenda” mbele ya rafiki na ndugu zake kwakuwa haoni sababu ya kuuficha ukweli uliopo nafsini mwake.

4. ANGALIA KAMA NI MUWAZI KWAKO.
Kama mtu anakupenda kwa dhati, daima atajitahidi kuwa muwazi kufunguka kwako kuhusu hisia zake, mawazo yake, kile anachokipenda, mambo asiyoyapenda, historia yake na hata matatizo yake binafsi. Hiyo yote ni ishara kuwa anakupenda hivyo yuko huru kukueleza chochote kwasababu anatambua kuwa wewe ni sehemu yake na hivyo basi una haki ya kutambua mazuri na mabaya yake yote.

 • Ukiona mtu wako anakwambia “Sijawahi mwambia mtu yeyote kuhusu jambo hili….” Ni ishara tosha kuwa anakupenda na anakuamini kiasi cha kukushirikisha siri zake.
 • Katika uwazi wake, kumbuka pia kuwa mtu anayekupenda hatoacha kukukosoa kwa busara pale unapofanya jambo kinyume na utaratibu, anafanya hivyo kwasababu anakupenda japo anatambua kuwa wanadamu si wakamilifu lakini anajua wazi ya kuwa anapaswa kukujunga katika msingi ulio bora kwasababu wewe ni baba au mama wa watoto wake, hivyo asipokukosoa ndivyo utakavyolirudia kosa hilo hata kwa uzao wenu.