August 3, 2017

Yajue matatizo 5 baada ya kutoa mimba.


Miaka ya hivi karibuni kumeongezeka vitendo vya utoaji wa mimba, hasa kwa kutumia madawa yenye kemikali, madawa ya kienyeji, hii imezidi sana haswa kwa nchi zinazoendelea ambazo nyingi zipo Africa ikiwemo Tanzania.

Wanaotoa mimba sana ni wasichana wadogo ambao wengi wanaanza kutoa mimba wakiwa kuanzia shule za msingi hadi kwa wale walioko vyuo vikuu ambao baadae hukumbana na matatizo makubwa kama ifuatavyo.

Isikupite hii: Dawa ya kutokwa na uchafu mweupe ukeni.  

1. Tatizo kuu la hatari zaidi ni kifo. 
Imekadiriwa kuwa karibu theluthi moja ya vifo vya kina mama ni kwa sababu ya utoaji wa mimba kwa njia isiyo salama. Kwa kila mwanamke anayekufa, imekadiriwa kuwa wanawake wengine 16 hadi 33 huwa na tatizo baada ya kutoa mimba kwa njia isiyo salama, pamoja na: Hemoreji (kutokwa na damu nyingi)

2. Maambukizi katika kaviti ya pelvisi, au katika mkondo wa damu. (kwa mfano, pepopunda) 
3. Kutoboka kwa uterasi (kushona mraruko wa kuta za uterasi kwa kifaa kilicho na ncha kali. Jerahi lililokaribu na ogani katika kaviti ya pelvisi (kwa mfano, uke, kibofu cha mkojo, rektamu na utumbo) 4. Sumu kutokana na dozi ya dawa iliyozidi kipimo chake au mitishamba inayotumiwa kutekeleza utoaji mimba wa kupanga. Hapo baadaye, 
5. Mwanamke anaweza kuugua kutokana na maumivu ya pelvisi yanayoendelea kwa muda mrefu (yanayojirudia), hasa wakati wa hedhi, mimba kutoka pekee yake unaojirudia au utasa.