Featured Posts

September 1, 2017

Mfahamu mwigizaji wa filamu ya yesu ambaye watu wengi hudhani kwamba ni yesu. (2)

Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye (Brian) azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon, akaamua kuzungumza nao, baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi.

Soma: Historia Fupi Ya Maisha Ya Rose Muhando.

Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto, lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.

Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani, na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa, shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.

Haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia, baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu, ukweli na kugusa mioyo ya watu.

Baada ya filamu hiyo Brian anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 133 (kwa takwimu za mwaka 2001), zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu, filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.

Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo, ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza, ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu.

Kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985, The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.

Soma: Historia Fupi Ya Maisha Ya Marehemu Askofu Moses Kulola.
Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel. Habari kwa msaada wa mtandao.