Featured Posts

September 1, 2017

Madhara 11 ya kunywa pombe (ulevi)

1. Kukosa raha  
Mtu akisha lewa huwa hana raha yoyote kwani hata akilala hujisikia kizunguzungu, huweza  kutapika na hata kukosa hamu ya kula chakula. Afya yake hupungua kwani anapoteza vyakula vingi. Maumivu makali hutokea sehemu za mbavu na kifuani na tumboni kwa kuwa misuli huwa haina nguvu kutokana na kuchoshwa wakati wa kutapika.

Isikupite hii: Dawa ya kutokwa na uchafu mweupe ukeni.

2. Ufukara
Mlevi husahau kununua mahitaji ya nyumbani ikiwemo nguo, chakula, vyombo na vinginevyo kwani fedha nyingi hutumika katika unywaji. Watoto hukosa chakula bora na hii huleta madhara mengi katika familia. Mtu akishiriki ulevi hawezi kufanya kazi yoyote, anakuwa mvivu na mzembe.

3. Ugomvi
Kutokana na kulewa watu hupigana na hata kuumizana. Watu wa namna hii hawaheshimiani kwani huwa hawana siri mbele ya watoto na ni aibu kubwa kwa wageni na watu wote. Mlevi hupenda kuharibu na hata kugawa vitu alivyonavyo hata vile ambavyo ni vya familia hivyo husababisha ufukara nyumbani.

4. Ajali  
Mlevi hupoteza akili na hata hajisikii kama ameumizwa vibaya. Haoni sawasawa na mwendo wake hubadilika. Vilevile anaweza kushindwa kabisa kutembea akalala popote barabarani au porini. Ajali nyingi hutokea kama kukanyagwa na gari, pikipiki, kuumwa na wadudu wakali kama nyoka na nge.

5. Magonjwa
Ukimwi, Kaswende, Kisonono, na mengine ya kuambukiza ni magonjwa ambayo mlevi anaweza kuyapata kwa urahisi kutokana na kufanya vitendo visivyo faa katika jamii pale anapokuwa amelewa. Anayefanya vitendo hivyo ni pombe sio yeye.

6. Kukosa kuzaa 
Ukishiriki Ulevi, sehemu nyingi za mwili hulegea sana hasa sehemu za viungo vya uzazi, kwani viungo huwa havina nguvu tena na mapato yake ni kuwa tasa.

Isikupite hii: Fahamu faida za pweza kwenye afya ya mwanadamu.

7. Uzembe 
Mtu mlevi huwa mzembe, hulewa tu kusahau na hata kudharau kazi yake. Mapato yake ni kufukuzwa kazi au kuachishwa kazi. Miradi yake husimama.

8. Kukosa afya nzuri
Pombe kama inazidi katika damu hufanya kazi ya kudhoofisha mwili. Watu wengi wakilewa hupoteza nguvu zao, hawapendi kula au wanakula kidogo sana. Pia hawapati chakula bora ikiwa fedha nyingi hutumika katika ulevi. Udhaifu wa mwili nao unaweza kusababisha magonjwa mengine ikiwemo kifua kikuu.

9. Matatizo ya moyo 
Hii ni shida kubwa ambayo inahitaji muda mwingi kukaa hospitalini ili kupata nafuu, wakati huo miguu na mikono huvimba pamoja na kupata matatizo katika mfumo wa upumuaji.

10. Figo 
Hushindwa kufanya kazi yake sababu mara nyingi huchoshwa na sumu ya pombe huku maini  yakishindwa kufanya kazi ipasavyo kutokana na kuzidiwa na kiwango kikubwa cha sumu kitokanacho na pombe.

Pia tumbo huvimba na kutokana na hatua hii maisha huwa ni mafupi sana. Kulewa kunaifanya mishipa ya fahamu kuharibika, kuumwa mwili wote na kukosa raha kabisa.

Isikupite hii: Faida 10 za mayai ya kuchemsha

11. Aidha pombe inaweza kusababisha upofu wa macho ambao hutokea baada ya mishipa ya macho kuharibika kwa kuwa haiwezi tena kupeleka mionzi inayofanya mtu kuona.