October 4, 2017

Historia fupi ya maisha ya Millard Ayo.

Millard Afrael Ayo alizaliwa Arusha January 26 akiwa ni mtoto wa kwanza kwenye famili ya watoto wanne ya Afrael Ayo ambae ni mmeru wa Akheri Tengeru, ni mfanyabiashara na mama Mary Ayo ni mwalimu.

Isikupite hii: Historia fupi ya maisha ya Mchungaji Antony Lusekelo, Mzee wa Upako.

Baada ya mama yake mzazi kuona uharaka wa uelewa wa Millard, alimuanzisha shule akiwa mdogo sana na hatimae kumaliza elimu ya msingi akiwa na miaka 12 tu, akamaliza form four akiwa na miaka 16 mwaka 2002, sehemu zote hizo yeye ndio alikua mdogo kuliko wote darasani kuanzia Patandi Primary School Tengeru, Akeri Secondary School na Mbezi beach high school.

Wakati akisubiri majibu, Millard alijiunga na Arusha College of Electronics na kusomea ufundi wa kutengeneza satelitte dish, tv deck na radio masomo ambayo aliyamaliza na aliyasoma kwa sababu ilikua ni kazi ya pili aliyoipenda, baada ya hapo mama yake mzazi alishawishiwa na marafiki zake ili Millard arudishwe shule kuendelea na masomo ya sekondari kitu ambacho alikikubali lakini hakikua na mapokezi mazuri kwa Millard kwa sababu yeye alihitaji kufanya kitu kingine kwa wakati ule.

Mambo yalibadilika pale uncle wake aitwae Gabriel aliekua Marekani aliporudi Tanzania na kumshawishi mama Millard amuache mtoto afanye kile anachotaka na anachokipenda, hapo ndipo Millard akapata nafasi ya kwenda kujiunga na East Africa Training Institute kusomea utangazaji na uandishi wa habari mwaka 2004.

Isikupite hii: Tabia 3 za watu wanaokubalika sana na jamii.

Baada ya mwaka mmoja Millard alijiunga na TVZ Zanzibar kwa muda wa miezi mitano na akarejea Dar es salaam April 2005 kutafuta kazi baada ya hali kuwa ngumu kwenye familia na kukosa pesa kwa ajili ya kujiendeleza na masomo.Tazama video: Je Goodluck Gozbert anatumia uchawi kuvuma kimuziki?