October 30, 2017

Tabia 10 za wanaume ambazo wanawake wengi huchukizwa nazo.

1. Kijana wa mama
Mwanaume wa aina hii wakati wote utamkuta kagandana na mama yake katika kilakitu kuanzia maongezi hadi matendo, hawezi kufanya chochote mpaka apate idhini kutoka kwa mama yake hata kama ana mke na maamuzi yanayofanywa ni ya kuihusu familia yake yeye. Katika familia ya mwanaume huyu mama yake huwa ndiyo mfalme katika kila kitu, yeye ndo ataamua mkae wapi, mjenge wapi, muende wapi, mlenini, na hata maamuzi mengine mkiyaamua ninyi basi yeye ataulizwa na mtoto wake ayakague kama ni maamuzi sahihi au la, na mara zote maamuzi yake ndiyo ya mwisho. Kwa mwanaume kama huyu kama wewe ni mke basi ufahamu mapema kuwa hata ufanyaje kamwe huwezi kuwa mzuri na mwema kama mama yake.

2. Mwanaume mvivu na mchungu:
Mwanaume wa jinsi hii ni kati ya wale ambao hawataki kabisa kujishuhulisha, wao hutaka kuwa na wanawake wenye kitu kama vile gari, nyumba, kazi nzuri n.k. utamkuta mwanaume wajinsi hii yeye ni kulala tu, kutaka kuzunguka na msichana wake tu, na kutegemea afanyiwe kilakitu kuanzia kununuliwa muda wa maongezi, usafiri, kupangiwa nyumba, mavazi n.k. Mkifika sehemu ya kula au kunywa na mwanaume wa jinsi hii basi uwe umejipanga kimfuko maana atakula na kunywa kwa bidii kama vile atalipa au atashiriki kulipa kumbe macho yake yote yako katika rehema za mfuko wako. Muepuke mwanaume wa jinsi hii kama ukoma.

3. Mwanaume msanii:
Hapa simzungumzii msanii kwa maana ya “Artist” bali namzungumzia mwanaume mwenye tabia za kisanii kama neno hili linavyotumika zaidi na wengi. Mwanaume wa tabia hii nirahisi wakati wote kuwa na mahusiano na wanawake tofauti hata pasipo wewe kujua, wananjia zao za kisanii kuikamata mioyo ya wanawake kadhaa kwa muda mmoja na wote kujiona wako salama kimapenzi mikononi mwa msanii huyu, ni ngumu sana kumgundua katika usanii wake na mara ukimgundua basi umeshaumia. Maranyingi hupenda kuvalia kiutanashati, wanajua kupangilia mapigo yao na hata rangi za kuvaa, ukimuona ni lazima utavutiwa nae na pia wao hufikiri kuwa wao ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa wanawake, utasikia wakati mwingi hadithi zao nijinsi walivyotakwa na kupendwa wanawake wengine na wakawakataa, wanafanya hivi kukuonyesha jinsi wewe ulivyo nabahati kuwa nao kumbe ni mojawapo ya usanii wao wa kilasiku

4. Mwanaume asiyepatikana “Mr Unavailable”
Wako wanaume ambao wao hudhani kuwa mapenzi yako katika uwezo wao wa kutoa mahitaji, yani usiseme huna simu, utanunuliwa mbili na ya akiba, usiseme huna muda wa maongezi, utatumiwa harakasana muda mwingi hadi utatamani kuuza salio, ikitaka akupangie nyumba kokote utakako haitamsumbua, ila tatizo linakuja pale wewe unapotamani kuwa nayeye muwe na muda wenu basi visingizio na sababu zinafululiza. Mtu huyu ataonekana tu pale ambapo anahitaji kufanya mapenzi na akimaliza tu anapotea na utamuona tena akihitaji wakati mwingine. Hili pia limewatokea wanawake wengi ambao wamejikuta wanaolewa au kuingia kwenye mahusiano na waume za watu, kamwe mume wamtu hawezi kuyafanya mahusiano ya kweli na yenye utoshelevu, lazima wakati wote ukubali luwa wa pili baada ya mke wake na watoto wake.

5. Mwanaume mwenye lawama juu ya maumbile yako:
Mwanaume wa jinsi hii maranyingi hujipenda mwenyewe au kwa maneno mengine ni mbinafsi, wakati wote anapenda uwe vile anavyowaza kichwani mwake hata kama haiwezekani, mara kwa mara utakuta analalamika sana kuhusu uzito wako, unene wako, ingawa unaweza kukuta hayuko tayari kukulipia kufanya mazoezi au basi kufanya mazoezi hayo na wewe, maneno yao ni kama; muone ulivyonenepa, unaongezeka kilo tu, unakula sana, umeridhika sana, n.k. najua maranyingine ningumu kumwambia unavyoumia lakini wanawake wengi huumizwa sana na masimango kama hiya, ukimwona anatabia hizi mapema jiepushe nae.

6. Mwanume asiyekubali kukua:
Wako baadhi ya wanaume waiotaka kuonyesha kuwa wamekuwa na kupevuka, wengine utawaona wamepevuka kimwili tu ila mawazo na matendo yao bado yanadhihirisha utoto walionao. Ukiangalia matumizi yao ya fedha ni katika vitu vya kitoto tu, unaweza kukuta hata muda wake mwingi atacheza michezo ya kompyuta “video games”, mara nyingine hata marafiki zake ni ambao bado hawajakuwa vizuri kiakili. Mwanaume wa jinsi hii atakuletea shida sana hasa katika kuwaza na kupanga mambo ya kimaendeleo hata kama leo unamuona anamapenzi motomoto.

7. Mwanaume mlaini:
Najua kwakusema mlaini simaanishi yuko kama karatasi au mpira bali asiyeweza kuwa imara na wakati wowote kuwa tayari kubeba jukumu. Hapa simaanishi mvivu, kwasababu mwanaume anaweza kuwa ma nguvu zake lakini mvivu, hapa namaanisha hata kimwili huyo mwanaume huonekana kama asiyeweza kazi, unaogopa hata kumwambia akusaidia kitu kwasababu mwili wake na muonekano wake tu umeshatuma ujumbe kuwa hawezi. Huyu atakukatisha tama mapema zaidi jaribu kumkimbia mapema tu.

8. Mwanaume ambaye ni bosi wako:
Najua wengi wetu tunawachukia mabosi wetu au wasimamizi wetu wa kazi ingawa wako wanawake ambao huenda hatua ya zaidi na kuanza mapenzi na mabosi hawa aidha kiuhalisi au kwasababu binafsi lakini maranyingi wengi wamekuja kuumizwa kwasababu maranyingine mapenzi baina ya watu hawa huwa hayadumu, na wengi huumizwa sana na maneno au skendo zinazoenea kama upepo kuhusu mahusiano waliyonayo na mabosi wao ingawa walianza kama siri nahivyo kushindwa kuendelea na mahusiano hayo. Kama kweli huna mapenzi ya kweli na hakuna ulazima basi jizuie kabisa kuzama kwenye penzi na bosi wako.

9. Mwanaume mwenye tabia za kike:
Kama mshauri wa kisaikolojia nimekutana na baadhi watu ambao wameingia kwenye mahusiano na wanaume ambao badala ya kuwa kama wanaume halisi wakawa kama rafiki mwingine wa kike wa karibu “girl friend”. Mwanaume wa aina hii utakuta anapenda kwenda na wewe kufanya manunuzi ya vitu kama nguo, marazote anatapenda akusikilize kilaneno unaloliongea, hata kama hachangii lolote, atatamani tu muwe wote na mfurahie muda wa kuwa wote. Angalia kwa makini unaweza kukuta unahusiana na mwanaume mwenye tabia za mahusiano ya jinsia moja “gay”

10. Mwanaume mwenye kupenda ngono sana:
Wako baadhi ya wanaume wenye uchu na ngono kila wakati na kila mahali. Haijalishi hatakama wewe ni mwanamke mwenye kupenda mapenzi sana au unavutia sana fahamu kuwa mwanaume wa namna hii lazima atafanya ngono nje ya mahusiano yenu mara atakapojisikia kukinaishwa na wewe na atafanya ngono na mwanamke yoyote atakayempata bila kujali kuwa sio mzuri kama wewe. Yamkini ni ngumu sana kumtosheleza kiu yake kwakuwa iko juu wakati wote, na hii inamaanisha mara tu utakapoomba kupumzika au unapoumwa kidogo basi fahamu kuwa hatoweza kuvumilia na anaenda nje. Wengi wa aina hii ya wanaume huwa na watoto wengi wan kwa je jinsi wasivyokuwa wavumilivu.