October 10, 2017

Tatizo sio hilo, tatizo lako ni mdomo wako.

Kuhama nyumba mnayokaa sio suluhisho la tatizo lako. Kuhama ofisi unayo fanyakazi siojibu la maswali yako, maana hata ukihama unahama na mdomo wako ambalo ndilo tatizo lako. 

Kwani nilazima uongee kila kitu? Hatakama unachokiongea umekisikia kwa mtu wakaribu swali ni je unauhakika wa unacho kiongea? Nikweli wewe ni kijana unae tokea vizuri kimwonekano lakini shida yako ni mdomo wako kaka, mdomowako unakunyima marafiki, majirani, unakunyima hata ndugu. 

Soma: Tabia 8 Za Watu Wapole - Dr. Chris Mauki.

Hata wewe mrembo, mwonekano wako ni mzuri kila mtu anatamani awe na wewe kwa mvuto wa umbo lako lakini shida yako ni mdo wako, unaongea sana. Chuja mambo kabla hujaongea. Chuja mambo yakusikia sikioni mwako. Chuja watu wakuwanao karibu. 

Wanasema ukimwona kuku kwa mganga ujue kaponzwa na rangi yake.