November 13, 2017

Je unajua maana ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ni nini (VAT)!!


Kodi ya Ongezeko la Thamani ni nini (VAT)

Kodi ya Ongezeko  la Thamani ni kodi ya mlaji inayotozwa katika bidhaa zinazostahili kutozwa kodi, ikiwa ni pamoja na huduma, mali zisizohamishika na shughuli yoyote ya kiuchumi wakati wowote thamani inapoongezeka katika kila hatua ya uzalishaji na katika hatua ya mwisho ya mauzo. Kodi ya Ongezeko  la Thamani  inatozwa kwa bidhaa zote zinazozalishwa ndani na huduma na kwenye maduhuli. Kodi ya Ongezeko la Thamani anatozwa mtu aliyesajiliwa kulipa Kodi ya Ongezeko  la Thamani  tu.

Mawanda ya Kodi ya Ongezeko  la Thamani  ni yapi?

Kodi ya Ongezeko  la Thamani  itatozwa katika usambazaji wowote wa bidhaa, huduma na bidhaa zisizohamishika za shughuli yoyote ya kiuchumi Tanzania Bara ambapo ni usambazaji unaotozwa kodi unaofanywa na mlipa kodi katika shughuli ya kiuchumi anayofanya. Uingizaji wa bidhaa zinazokatwa kodi kutoka sehemu yoyote nje ya Tanzania Bara zitatozwa Kodi ya Ongezeko  la Thamani  na Sheria za Kawaida za Forodha na taratibu zitatumika. Bidhaa zote zitakazotumika nje ya Tanzania Bara hazitatozwa Kodi ya Ongezeko  la Thamani  baada ya kupata uthibitisho. Kodi ya Ongezeko  la Thamani  itatozwa kwa bidhaa na huduma zinazotozwa kodi. Viwango sanifu vya Kodi ya Ongezeko  la Thamani ni 18% na 0% kwa bidhaa zinazosafirishwa nje ya nchi.

Usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani 

Usajili wa  Kodi ya Ongezeko la Thamani ni lazima kwa kila mtu aliyefikia kiwango cha juu cha usajili cha milioni 100 kwa kipindi cha miezi 12 na zaidi au milioni 50 kwa kipindi cha miezi 6 kinachoishia katika miezi iliyopita. Sharti hili linahusu aina zote za usajili isipokuwa kwa watoa huduma za kitaalamu.

Mchakato wa Usajili

Maombi ya usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani yanaweza kufanyika mtandaoni au kwa kujaza fomu ITX245.02.E Maombi ya Usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani.

Cheti cha Usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani

Kufuatia usajili, mlipakodi atapewa cheti cha usajili kikitaja jina na mahali ambapo ilipo biashara ya  mlipakodi, tarehe ambayo usajili umefanyika  na namba ya utambulisho wa mlipakodi na namba yake ya usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani.

Mtu huyo ataonesha namba ya utambulisho wa mlipakodi na namba yake ya usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani katika taarifa yoyote, hati ya rufaa au nyaraka nyingine zinazotumika kwa shughuli rasmi Zinazohusu Kodi ya Ongezeko la Thamani na kutundika cheti chake cha usajili katika sehemu ambayo inaonekana kwa urahisi katika eneo lake la biashara

Jisajili mtandaoni kwa kubofya hapa.


Taarifa ya VAT na Malipo ya Kodi

Taarifa ya VAT ni fomu inayotumika kuwasilisha malipo ya kodi kwenda Mamlaka ya Mapato. Kwa sasa wafanyabiashara waliosajiliwa katika VAT wanatakiwa kuwasilisha taarifa zao za mapato katika ofisi za Mamlaka ya Mapato kwa njia ya mtandao.

Taarifa ya VAT inatakiwa kujazwa na kuwasilishwa kwa Kamishna Mkuu si zaidi ya tarehe 20 ya kila  mwezi baada ya mwezi wa biashara pamoja na malipo ya kodi yoyote kama ipo.


Taarifa ya VAT mtandaoni Bofya hapa kuweza kutuma VAT Returns kwenda TRA

Bofya hapa kupata Maelekezo ya jinsi ya kutuma VAT returns 


Kwa msaada zaidi kuhusu Ongezeko la kodi ya dhamani wasiliana nasi kupitia +255769360989/+255625596236  tutakufahamisha zaidi.

Pamoja Tunajenga Taifa Letu.