November 19, 2017

Mambo 11 usiyoyajua kuhusu Dkt. Luis Shika.

Dkt. Luis Shika ni jina ambalo linaotrendi sana katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, tumesahau kusuhu Lissu, ACACIA  na Mh. Magufuri, mmmmhh... Kati interview nyingi ambazo Dkt. Luis Shika ameitwa na kuhojiwa amefunguka na kusema mengu sana kuhusu maisha yake. Na haya  ni mambo 11 usiyoyajua kuhusu Dkt. Luis Shika.

1. Dkt. Luis shika alipata degree yake ya kwanza mwaka 1991 baada ya kusoma miaka 7 huko Urusi. 

2. Alipata degree yake ya pili mwaka 1993 huko huko Urusi. 

3. Dkt. Luis Shika ni daktari wa binadamu. 

4. Baada ya kumaliza degree yake ya pili, aliongeza nyingine ya tatu yani PHD na kisha akaongeza 1 nyingine. 

5. Dkt. Shika ni msomi wenye degree 4 na baada ya kumaliza alianza kufundisha katika chuo kikuu kimoja huko urusi. 

6. Tarehe 28/07/1999 Dkt. Luis Shika alifungua kampuni yake inayohusika na utengenezaji wa kemikali za viwandani na mashambani. 

7. Baada ya uchumi wa Urusi kuporomoka Dkt. Luis Shika alinunua viwanda vingine 10 huko urusi. 

8. Baada ya kuonesha mafanikio makubwa sana huku Urusi, mwaka 2004 alitekwa nyara na watu wasiojulikana wakitaka awape dollar za kimarekani millioni 1.2.

9. Alifanikiwa kutoroka na kusaidiwa na ubarozi wa marekani katika matibabu n.k na hata siku moja hakuwahi kutembelewa wala kusaidia na ubarozi wa Tanzania.

10. Baada ya hapo alirudi nchini Tanzania na kisha kuelekea nchini ispania ili kuyaokoa maisha yake kwa sababu waliomteka waendelea kumtafuta. 

11. Dkt. Luis Shika anahusiano mzuri wa kimataifa na ubarozi wa nchi ya Marekani kuliko Tanzania. 

Tazama video: Masanja Mkandamizaji akimuigiza Magufuli.