November 1, 2017

Mambo 40 yanayopelekea kuvunjika kwa mahusiano ya ndoa.

1. Kutokuwa na mawasiliano ya karibu na mwenzi wako.
2. Kutojali maumivu ya mwenzi wako.
3. Ubishi usiokuwa na maana.
4. Kupenda kujihesabia haki.
5. Kutokubali makosa.
6. Kutokuwa na roho ya msamaha.
7. Kutokuwa muwazi kwa mwenzi wako.
8. Usaliti wa mapenzi.
9. Kuigiza kupenda.
10. Kutomheshimu mwenzi wako.
11. Kuwa mjuaji kila kitu unajifanya unajua.
12. Kutokutambua uthamani wa mwenzi wako katika maisha yako.
13. Kuwa na jeuri/kiburi
14. Kutokuwa na kifua cha kuficha mambo ya nyumbani/ndani
15. Kutojali watu wa nyumbani kwako {ndugu,watoto n.k}
16. Kujiamulia kufanya vitu bila ushauri wa pamoja.
17. Kutojua jinsi ya kumfariji mwenzi wako
18. Kutomridhisha mwenzi wako kimapenzi.
19. Kuwa na amri kama bosi na mtumishi wake.
20. Ugomvi wa muda mrefu usiokuwa na suluhu.
21. Kuwa na ahadi za uongo.
22. Kumdhalilisha mwenzi wako mbele za watu.
23. Kupenda starehe kuliko kujenga upendo wa kudumu
24. Uchafu {kutojipenda na kupenda mazingira yako}.
25. Maudhi ya mara kwa mara.
26. Kutoonyesha hisia kali za mapenzi kwa mwenzi wako.
27. Kutokuwa karibu na mpenzi wakati wa dhiki
28. Kutokuwa mbunifu wa maisha ya kimapenzi.
29. Kutokuwa na msimamo katika maamuzi yako
30. Kutokuwa na muda na mwenzi wako.
31. Kutokuwa na shukrani.
32. Kutokujua gharama za upendo.
33. Kuwa na wivu wa kijinga.
34. Kuwa mbinafsi.
35. Kujifanya busy na kushindwa kuhudumiana kimatamanio
36. Kutokuwa na imani juu ya mwenzi wako.
37. Kutokubaliana na hali halisi ya maisha yenu.
38. Kutokukubali kujifunza.
39. Kutokutambua maana ya mapenzi na umuhimu wake.
40. Kutokuwa wacha MUNGU/ Khofu ya MUNGU