November 19, 2017

Mtindo huu wa kufanya mapenzi unawapoteza mamilioni duniani - Utafiti.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa ripoti mpya kuhusu hali ya afya ya uzazi likieleza kuwa ngono kwa njia ya mdomo imeendelea kuwa tishio kubwa kwa usambazaji wa magonjwa ya zinaa na kupelekea hata kutotibika.

Uchambuzi wa WHO umeeleza kuwa taarifa zilizokusanywa katika nchi 77 duniani zimeonesha kuwa magonjwa ya zinaa ya gonorrhea yaliyoambukizwa kwa kushiriki ngono kwa midomo (oral sex) yamekuwa yakipambana vikali na dawa kusambaa kwa haraka zaidi.

Dk. Teodora Wi, wa WHO  ameeleza kuwa kumekuwa na kesi tofauti katika nchi za Japan, Ufaransa na Uhispania ambapo maambukizi ya magonjwa hayo ya zinaa yamekuwa hayawezi tena kutibika.

Ameeleza kuwa aina hiyo ya ngono inasambaza kwa kasi bakteria wa magonjwa hayo ya zinaa na kwamba upungufu wa kondom katika nchi kadhaa pia umesaidia katika usambazaji huo.

Mtaalam huyo wa WHO amesema kuwa utafiti huo umeonesha kuwa takribani watu milioni 78 duniani kote hupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa kila mwaka, na kwamba dawa za kupambana na magonjwa hayo zimekuwa zikizidiwa nguvu.

“Gonorrhea ni mdudu mjanja sana, kila tunapozindua aina fulani ya tiba kuitibu, mdudu anazidi kuongeza nguvu za kuishinda tiba hiyo,” BBC inamkariri Dk. Teodora Wi.

Alisema kuwa kwa bahati mbaya maambukizi mengi ya gonorrhea yako kwenye nchi zinazoendelea ambapo ni ngumu zaidi kubaini dalili za ugonjwa kwa haraka.

Tazama video: Majaribu ofisi ya Mchungaji, nyie wadada Mungu anawaona!