November 12, 2017

Jinsi ya kutambua kama ni mtoto wa kike/kiume wakati wa ujauzito?

Tumbo
Wazoefu wanaamini kuwa endapo utakuwa umebeba uzito mdogo tumboni na tumbo dogo mtoto atakuwa ni wa kiume.

Chunusi 
Uwepo wa chunusi nyingi na mara kwa mara ni ishara kuwa umebeba mtoto wa kiume wakati ngozi kuwa laini sana kupita awali ikimaanisha ni mimba ya mtoto wa kike.

Haja ndogo 
Endapo mama mjamzito anatoa haja ndogo rangi nyeusi kuna uwezekano mkubwa amebeba mtoto wa kiume huku nyeupe au rangi ya mawimbi ikimaanisha jinsia ya kike.

Isikupite hii: Hizi ni njia 5 za kupambana na msongo wa mawazo.

Miguu
Kuwaka moto na kuwa laini ina maanisha mimba ya mtoto wa kike wakati miguu kuwa na mikono ya baridi ni mtoo wa kiume.

Mapigo ya moyo 
Hii hutumiwa na wataalamu wa afya ambapo mapigo chini ya 140 ni mtoto wa kiume na ikiwa ni zaidi ya 140 ni mtoto wa kike.

Nywele
Mwanamke anapokuwa mjamzito na nywele zikaota au kukua kwa kasi inamaanisha mtoto aliyenae tumboni ni wa kiume wakati kinyume chake ni jinsia ya kike.