• Isikupite Hii

  November 19, 2017

  Vichocheo vya maamuzi - Nguvu ya Maamuzi (Part 12)

  Mtu anapofanya maamuzi mazuri au mabaya ni matokeo tu; vipo vitu kadha wa kadha vinavyompelekea mtu kufanya maamuzi anayoyafanya vitu hivyo huitwa vichocheo vya maamuzi  

  Vichocheo vya maamuzi;
  •  Tamaa mbaya; tamaa ni msukumo wenye hamasa ya kupata kitu Fulani,  tamaa huwa mbaya pale ambapo msukumo huo unakupelekea kutumia njia isiyo halali ili kupata kitu hicho unachokitaka  kwa mfano; unatamani kuwa na maisha ya aina Fulani ama uchumi wa ina Fulani  unatamani ujenge nyumba ya kifahari utembelee gari ya thamani kubwa, tamaa humtengenezea mtu wazo ( idea) namna ya kufanya ili kutimiliza tamaa yako  wazo hilo linapopata  ushawishi mkubwa mtu anafanya maamuzi ya utekelezaji wa wazo hilo, tamaa huweza kuchochewa na vitu unavyoviona, unavyovisikia, unavyovisoma n.k .Tamaa imechochea watu wengi sana  kuingia kwenye dhambi ya uzinzi na uasherati, rushwa na ufisadi, utapeli na biashara haramu  kama vile ukahaba na dawa za kulevya  ili tu kupata vile wanavyovitamani.
  •    Marafiki  na watu wa karibu  ; marafiki  wana nguvu kubwa sana ya ushawishi  kwani ni watu wa karibu yako wanaokushauri na kukusaidia kwenye mambo yako mengi  Uzuri ama ubaya wa maamuzi yako uatategemea pia aina ya marafiki ulionao . marafiki wabaya; watakushawishi katika vitu vibaya, watakupa ushauri mbaya, mambo haya yatakupelekea ufanye maamuzi mabaya. Watu wa karibu ni watu wale unaowaamini, unaowashirikisha mambo yako  wenye nguvu ya kukushawishi na kukushauri pia,mfano wazazi ama walezi ,washauri wa kiroho, mke au mume, ndugu n.k  ili kuwa na maamuzi mazuri  ni lazima  uwe makini katika kuchagua marafiki wa kuambatana nao , pia ni vema kuwa makini katika kuchambua ni yupi anafaa kumshirikisha jambo lipi,pia ni lazima kupata muda wa kutosha kutafakari kila ushauri  na ushawishi  kutoka kwa watu wetu wa karibu ili kujilinda dhidi ya maamuzi mabaya
  •  Utamaduni ;utamaduni umechochea maamuzi ya  wengi  kuna tofauti mbali mbali za tamaduni kulingana na koo mbali mbali, ama tofauti za makabila,ama  lugha, nchi n.k.  Jambo ninalotaka ujue ni kwamba si kila tamaduni ni nzuri baadhi ya tamaduni ni mbaya na hazifai kabisa kuathili mifumo yetu ya kufikiri; mfano kuna watu wanalazimika kuoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa sababu tu utamaduni wao unawataka kuoa ama kuolewa na watu wa kabila lao.  usifanye maamuzi kwa sababu tu utamaduni wako ama kabila lako linakutaka ufanye hivyo. Madhara ya kila maamuzi unayofanya ni juu yako wewe, kwa sababu unawajibika kulipa gharama ya kila maamuzi unayofanya.
  • Mtazamo; pia ni kichocheo cha kipekee sana  aina ya maamuzi ya mtu yatategemea pia mtazamo  alionao na namna anavyoyachukulia mambo.  Mtazamo unaopelekea maamuzi mabaya ni mtazamo( hasi) mtazamo ambao umejawa na hofu na woga mtazamo ambao wakati wote  hufikiri  matokeo mabaya . Mtu mwenye mtazamo wa aina hii hawezi kufanya maamuzi mazuri kwani kila jambo zuri hulifikiri kwa namna mbaya; mtu huyu akitaka kufanya biashara hufikiri zaidi kuhusu hasara kuliko faida , akitaka kuoa ama kuolewa huwaza zaidi matatizo ya ndoa kuliko faida . mtazamo wa aina hii unaua imani na kupofusha macho kuona fursa mpya na kuona uwezekano .ili kuwa na maamuzi mazuri ni lazima kuchukua hatua za kubadilisha mitazamo yetu na namna tunavyoyachukulia mambo.

  • Vitu tunavyoambatana navyo kwa kuona na kusikia;hivi ni vitu tunavyopendelea kuviona na kuvisikia  kwa mfano  majarida na vitabu mbalimbali tunavyopendelea kuvisoma ,program za TV tunazopendelea kutazama , aina ya vitu tunavyopendelea kuvitazama na kuvisikiliza kwenye internet , vitu hivi ni kichocheo kikubwa sana kinachopelekea maamuzi yetu kwa sababu vitu hivi hujaza nafsi zetu na fahamu zetu  na  kututengenezea aina ya mtazamo na namna tunavyochukulia mambo, vitu hivi ndivyo hufanyika kiini cha maamuzi yetu kwa hiyo maamuzi yako yatategemea nini kimejaza fahamu zako na nafsi yako. Ni lazima kuwa makini sana kwani vitu vibaya vimetawala zaidi na vinanguvu zaidi ya ushawishi  kuliko vitu vizuri.  Watu wengi huambatana na vitu ambavyo havina tija kwenye maamuzi yao hivyo kuwatengenezea maamuzi mabaya, kwa hiyo ukitaka kubadilisha aina ya maamuzi yako ni lazima uwe makini kuchagua vitu vya kuambatana navyo.

  •  Uhitaji; ni moja kati ya chachu mbaya ya maamuzi , mara nyingi mtu anapokuwa kwenye uhitaji huangalia zaidi namna ya kupata kile anachokihitaji  bila ya kujali madhara ya njia wanayotumia kupata vile wanavyohitaji ,unahitaji kazi,unahitaji mtoto, unahitaji ada ya shule n.k.usifanye maamuzi tu kwa sababu ya kupata kile unachokihitaji ni lazima uangalie maamuzi unayotaka kuyafanya kama ni sahihi, kwa sababu madhara ya maamuzi hayo huweza kuwa ni makubwa zaidi kuliko hata uhitaji wako wa sasa.

  •  Kutishiwa ama kulazimishwa; hali hii hutokea mara nyingi hasa pale mtu anapokuwa kikwazo kwenye jambo ambalo lina maslai kwa watu Fulani, ama wakati mtu anataka umtimizie haja  Fulani ambayo hukubaliani nayo. Kutishiwa ama kulazimizwa  huweza kufanywa na watu wenye ushawishi Fulani kwenye maisha yetu kwa mfano  boss anamlazimisha jambo Fulani mfanyakazi wake, mume anamlazimisha jambo mke wake , mzazi anamlazimisha jambo mtoto wake,wafanyakazi wanamlazimisha jambo mfanyakazi mwenzao, mchungaji anamlazimisha jambo muumini wake  n.k. Mara nyingi inapotokea hali ya kulazimishwa jambo na ukaonekana umeshikilia msimamo wako vitisho hutumika  vitisho vya kufukuzwa kazi ,vitisho vya kutengwa ,vitisho vya talaka, vitisho vya kufukuzwa nyumbani n.k. Usifanye maamuzi mabaya ili tu  kuwalidhisha wanaotaka ufanye maamuzi hayo . simamia  msimamo wako, linda imani yako  na thamani yako kwa sababu wewe ndiye utakaye wajibika  na matokeo ya maamuzi hayo.

  • Mfumo wa maisha; mfumo wa maisha  una mchango mkubwa sana kukufanya uwe na maamuzi  mabaya ama mazuri,mfumo wa maisha ndio unaoamua sehemu unazopendelea kwenda, aina ya watu unaokutana nao,matumizi yako ya kila siku, mfumo wako wa maisha pia ndio unaokutengenezea  vipaombele ukitaka kuwa na maamuzi mazuri ni lazima uchague mfumo wa maisha ambao utakuwa chachu ya maamuzi  mema kwako. Ili mfumo wako wa maisha ukufae ni lazima;
  •  uwe ni ule unaokuweka karibu na Mungu wako yaani unaboresha mahusiano yako na Mungu wako,
  •  lazima pia uwe ni mfumo unaoendana na kipato chako; usiishi maisha ya kuigiza ukiishi maisha tofauti na kipatochako utaishia kuwa mtu mwenye madeni  na hautafuraia maisha yako.
  •       mfumo wako wa maisha pia ni lazima ukupe mwendelezo wa utimilifu wa maono yako na ukufanye uishi sawa sawa na kusudi la kuishi kwako. 
  •  Pia kuna umuhimu mkubwa sana kuhakikisha mfumo wako wa maisha unalinda msimamo wako na imani yako na inaenda sawa sawa na  mtazamo wako kuhusu maisha 

  Yupo ambaye akitoka kazini anakwenda nyumbani kukaa na familia yake wakati huo huo yupo ambaye akitoka kazini anakwenda bar. Yupo ambaye hutumia weekend kujiweka karibu zaidi na Mungu wake na kushughulikia matatizo ya jamii yake. wakati huohuo mwingine hutumia weekend kwenye majumba ya starehe akilewa na kufanya mambo ya anasa Mifumo tofauti tofauti ya maisha huamua aina ya maamuzi tuliyonayo.

  INAENDELEA……………………..
  EMMANUEL MWAKYEMBE (MR. YOPACE)
  Mobile: +255716531353
  Email: emamwakyembe@gmail.com