December 31, 2017

Breaking News: Whatsapp imeacha kufanya kazi sasa kwa Mataifa mbalimbali Duniani.

Mtu wangu wa nguvu nikusogezee taarifa kuhusiana na Mtandao wa Whatsapp leo December 31, 2017 umekuwa chini kwa mamilioni ya watumiaji ulimwenguni kote, na kusababisha hofu kwa kwa watumiaj hasa kwenye kipindi hiki wakati watu wa nguvu wakiwa wanasubiri Mwaka Mpya.

Watumiaji nchini Uingereza , Barbados, India, Japan, Panama, Afrika Kusini, Hispania, na Qatar wamesema hawakuweza kuungana na programu hiyo kwa kutuma meseji au kupokea wala kuweka Status.

Programu hiyo maarufu ya ujumbe ilitoa tangazo mapema wiki hii na kuelezea kuwa inatazamia kuwa mahiri kwenye mfumo wa iOS na Android kitu ambacho watalaam wanasema kinaweza kuwa kimechangia usumbufu huo unaojitokeza sasa.

“Tunapotarajia  miaka saba ijayo, tunataka kuzingatia jitihada zetu kwenye ambazo simu idadi kubwa ya watu hutumia,” kampuni hiyo imesema katika  majarida mbalimbali.

Mapema kampuni ya Tech imetangaza kuwa kifaa chochote cha BlackBerry kinaendesha BlackBerry OS au BlackBerry 10 hakitatumia tena programu ya ujumbe wa Whatsapp kwa mwaka 2018