December 7, 2017

Zifahanu faida za kusoma kwa njia za mitandao.

Kukua na Kuongezeka kwa teknolojia, kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi duniani hivyo basi hata elimu namna ya kuipata imebadilika. Unaweza kusoma kwa njia ya mtandao na haulazimiki kwenda chuoni kila siku au mara kwa mara ilimradi uwe na komputa yenye intaneti. Ingawa watu wamekuwa wakiichukulia kwa ugumu kidogo ukilinganisha na kuhudhuria darasani kila siku, wanafunzi wanaosoma kwa njia ya mtandao wanaonyesha kuridhika zaidi na elimu zao na hufanya vizuri zaidi kwenye matokeo yao.

Kusoma kwa njia ya mtandao kuna faida nyingi, zifuatazo ni baadhi tu:

1. Urahisi wa kusoma
Inawezekana watu wengi wanapenda kusoma kwa njia ya mtandao hasa hasa nchi zilizoendelea ni kwasababu ya urahisi wake wa kusoma. Mwanafunzi anapata faida asomee wapi saa ngapi na lini. Haimaanishi masomo ni mepesi , hii inamaanisha hautatakiwa kwenda darasani kwa muda maalumu kitu ambacho kinasaidia watu wenye familia au wanaofanya kazi ambazo zinawabana sana. 


2. Uwezo wa kupata masomo kwenye mtandao
Kitu unachohitaji ni komputa na intaneti tu, hivyo unapata na kuweza kusoma kitu alichofundisha mwalimu kwa njia ya video, sauti na hata nakala za maandishi ya kawaida. Mfumo huu unakufanya kurudia kitu kama hujaelewa na hupotezi kitu, kuliko madarasa ya kawaida mwalimu akishafundisha ukisahau na kama hukuandika inakuwia vigumu kukumbuka alichokisema au alichoelezea. 


3. Mawasiliano na mwalimu wako
Mwalimu siku zote anapatikana kwa njia ya barua pepe au simu, hautasubiri mpaka umfuate ofisini au masaa ya kazi. Vilevile unapata matokeo yako haraka kwa kuwa kila kitu unakifanya kwa njia ya mtandao. Hivyo inakuongezea kuwajibika na unakuwa unajua mwenendo wa masomo yako mara baada ya kumaliza kufanya mazoezi ya somo au majaribio ya somo. 


4. Gharama zake ni ndogo
Gharama utakayo lipa ni ada tu ya mwaka, ambayo inakuwa rahisi kuliko elimu ya kawaida ya kuingia darasani. Vilevile hutahitajika kulipia vitu kama vitabu, hosteli, gharama za kujiandikisha n.k 

5. Huna ugomvi na mwalimu au mkufunzi wako
Zile tabia za mwalimu kumfuatilia mwanafunzi, kwa njia ya mtandao ni ndogo au hamna kabisa. Hivyo msongo wa mawazo wa kupunjana maksi kwa sababu ya mambo binafsi na mkufunzi hayapo.