December 6, 2017

Kweli 15 usizo zijua kuhusu mahusiano ya muda mrefu.

1. Lazima ujue kwamba upendo hata kama mkubwa kiasi gani kuna siku mtakutana na changamoto kubwa na ngumu katika maisha na mahusiano yenu.

2. Sio kila wakati utampenda mwenzi wako.

3. Sio kila wakati utaweza kumvutia mwenzi wako.

4. Sio kweli kwamba mtaweza kufanya tendo la ndoa kwenye ubora wake na kuridhisha mwenzi wako kila siku.

5. Nyakati za uchungu zipo.

6. Mtakosana na kuumizana.

7. Sio kweli kwamba utakuwa sahihi wakati wote na mwenzi wako ndiye atakuwa anakosea.

8. Utapoteza uaminifu kwa mwenzi wako naye pia.
Uaminifu ndiye bidhaa hadimu na yenye dhamani kubwa kuliko bidhaa zote hapa dunia, inachukua muda, pesa, nguvu, mawasiliano n.k kujenga uaminifu lakini kitendo cha sekunde moja tu unaweza kubomoa uaminifu.

Unapopoteza uaminifu kwa mwenzi wako, usimlaumu wala usimwone ni mtu mbaya lakini anza kujenga upya misingi ya uaminifu. huwezi kuja kwanga na ukaniomba nikuamini lazima nikaye na wewe ili nikuchunguze kisha nidhibtishe kwamba naweza kukuamini.

9. Jifunze kumeza kuburi chako. Mara kwa mara

10. Tambua kwamba mwenzi wako atabadirika, atageuka na kujiendeleza baada ya muda flani. Mara zote.

11. Jifunze kukubalina na ubora umzri na mbaya wa mwenzi wako.
Kuna vitu atafanya kwa ubora na utavipenda lakini pia kuna vina atafanya kwa viwango vya chini jifunze pia kumfurahi na kukubaliana na vitu hivyo kisha ukimfunza kwa upendo na mbinu sahihi ili afanye kwa ubora sahihi.

12. Utagomabana.

13. Hakikisheni mnakula chakula cha usiku kwa pamoja.

14. Hakikisha mchaza na kuwa na wakati mzuri pamoja.

15. Jifunze kutaniana kucheka katika utani/vichekesho vyenu.