December 9, 2017

Mambo ya kuzingatia ili kupata mapenzi ya kweli.

Wiki hii Tunaongea kuhusu watu wale waliovunjika moyo katika swala nzima la mapenzi.

Siku zote hakuna kitu kinachouma sana kama kupenda sehemu ambayo unaamini utapenda kama upendavyo wewe, lakini kitu kinachoumiza zaidi ni kumpenda mtu halafu asijue au asiheshimu thamani ya penzi lako kwake.

Mara nyingine inawezekana Mungu anataka tukutane na watu ambao sio sahihi kwanza ili tukikutana wa watu waliosahihi, ili tujue jinsi ya kutunza au kuthamini na kujivunia zawadi hiyo kwasababu tunaamini ukifika mahali ukampata mtu uliyekuwa unamtafuta hiyo ni zawadi tosha.

Kitu kinachosikitisha ni kukutana na mtu anayemaanisha kweli kwako, lakini inawezekana kutokana na kuumizwa mara nyingi na kuvunjika moyo, unamuacha aende, bila kuchunguza, ni vizuri kuchunguza kabla ya kuacha au kuanza mahusiano mapya.

Naamini mlango wa furaha ukifungwa, mwingine hufunguliwa lakini mara nyingi huwa hatujui thamani ya kitu tunachopata na pengine kwa kile tulichonacho mpaka pale tunapokipoteza na pia hatujui ni kitu gani tunakikosa mpaka pale tunapokipata.

Kumpa mtu mapenzi yako yote haimaanishi kuwa atakupa na kukupenda kama vile vile unavyompenda, kitu cha kuzingatia ni kuwa kama umeamua kupenda, usipende kwasababu unategemea kitu flani, penda, muamini na uzibe masikio maana mara nyingi wengi wetu huwa kwenye mkandamizo pengine kutoka kwa ndugu na marafiki. Ukifanya hivyo mambo mengi unaweza kuyaepusha kwa kutosikia maneno yao kwa sababu mara nyingine mdomo huchangia kuvunjika kwa mapenzi.

Mara nyingi vitu unavyotegemea kuvisikia kwa mtu Fulani hautavisikia kutoka kwake lakini hii inategemea na wewe mwenyewe umeshawahi kumwambia unapenda kusikia kitu gani kutoka kwake? Umeshawahi kumwambia unampenda? Au kumzoesha hivyo?

Yapo baadhi ya mahusiano kutumia neno nakupenda hata mara moja kwa miezi ni tatizo, au unaweza kumwambia mpenzi wako NAKUPENDA akakujibu najua, au nani asiyejua unanipenda!  Kama una roho nyepesi unaweza ukalia  na kesho huwezi kumwambia tena,.

Unaweza ukafanya maamuzi halafu baadae ukayajutia, usiseme kwaheri kama unajisikia kuendelea,  usiseme humpendi mtu tena kama unajua huwezi kumuacha aondoke lakini pia usiseme huwezi tena kama unadhani unaweza kujaribu kwasababu siku zote mapenzi huja kwa wote ambao bado wana tumaini/wanaamini.

Kwa wote ambao walishawahi kuumizwa, wale walio wahi kusalitiwa, kwa wote wanaohitaji mapenzi/kupendwa, wote walioangushwa kimapenzi kabla na kwa wote ambao wapo tayari kuamini na kufuta imani kuwa hakuna mapenzi ya kweli au kama wanawake wanavyosema  wanaume wote baba mmoja na mama mmoja na kwa wanaume wanasema wanawake mwalimu wao ni kipofu.

Kumbuka inachukua dakika kumuona mtu na saa kutamani, siku kupenda lakini inagharimu maisha kumsahau mtu uliyempenda kutoka moyoni.

Usiwe na mtu kwasababu utapata kitu flani ua kwasababu jamii itakuangalia kwa sura flani, kuwa na mtu anayekufanya uwe na furah akwasababu itagharimu tabasamu tu, kutengeneza na kufanya siku zako ziwe nzuri na mwonekano wenye mwanga.