December 2, 2017

Unajua ni kwanini Masanja Mkandamizaji ni tajiri? Siri iko hapa (+Picha10)

Msanja Mkandamizaji ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Mgaya ni mchekeshaji, mjasiriamali, mwimbaji na pia ni mchungaji. Watu wengi walimfahamu kwa jina la Masanja Mkandamizaji alipokuwa akichekesha katika kipindi cha Orijino Komedi kilichokuwa kikirushwa na TBC.

Tazama: Picha 4 Za Mishe Mishe Za Masanja Mkandamizaji Akisaka Pesa Mtaani.

Hivi karibuni karibu amejiingiza kwenye masuala ya kilimo ambapo sasa amekuwa akitengeneza fedha nyingi kupitia kilimo. Masanja anakadiriwa kuingiza kiasi cha kati ya shilingi milioni 200 hadi 350 kutokana na kilimo.

Achia mbali Masanja, vijana wengi sasa wamekuwa na mwamko wa kujiingiza katika kilimo cha kisasa na kuweza kuwaajiri watu na kujitengenezea kipato kupitia kilimo. 
Kilimo sasa kimeonekana kuwa ni moja ya sekta ya ajira na si adhabu au kazi ya kufanya pindi unapokuwa huna kitu kingine cha kufanya kama livyokuwa inadhaniwa.