December 1, 2017

Pilipili husaidia kukata tabia ya kula chakula chenye chumvi nyingi - Utafiti.

Umewahi kuwa au kukutana na watu ambao ukifika wakati wa kula kabla hata hawajaonja chakula ili kujua kiasi cha chumvi au sukari kilichopo kwenye chakula hicho, huongeza kabisa chumvi au sukari ndipo waanze kula?

Hili tatizo la kuongeza chumvi kwenye chakula baada ya kupikwa limetajwa kuwa na athari nyingi kiafya lakini hata hivyo wataalamu wanasema hakuna matibabu an dawa ya kukomesha hamu hiyo ya chumvi au sukari zaidi kwenye chakula.

Wataalamu kutoka Bowling Green State University Marekani wameeleza kuwa kutumia pilipili kwenye chakula au viungo vya kupikia vyenye pilipili husaidia kukata hamu ya kula chumvi nyingi kwenye chakula na hii huepusha madhara yanayotokana na tabia hii.