December 30, 2017

Tatizo la kuumwa u.T.I kila mara na tiba.

U.T.I ni neno la kiingereza linalotamkwa kwa kifupi lakini kirefu chake ni, "Urinary Tract Infections" likimaanisha, "Maambukizi katika njia ya Mkojo"

Ugonjwa huu humpata mtu yeyote bila kujali jinsia au umri.

VISABABISHI VYAKE
Ugonjwa wa U.T.I unaweza kusababishwa na vijidudu vya namna nyingi. Bakteria aina ya Escherichia Coli kwa kiasi kikubwa ndo wanaosababisha ugonjwa huu wa japo bakteria wengine wapo.
Upande wa wanawake, tatizo la fangasi katika sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana. Uwepo wa fangasi hasa kwenye uke na maeneo jirani pia huweka mazingira ya mvuto kwa bakteria kuvamia maeneo hayo na kuleta maradhi ya UTI.
Kwa wanaume kutokana na maumbile yao na mfumo mzima wa mkojo na viungo vyake, hawa siyo waathirika wakubwa wa tatizo hili.

DALILI ZA U.T.I
Dalili za huwa kama ifuatavyo:
1. Kusikia maumivu wakati wa kukojoa.
2. Kuhisi homa
3. Kuhisi uhitaji wa kukojoa mara Kwa mara na pia mkojo kuwa na hali ya kuunguza wakati wa kukojoa
4. Kuhisi maumivu ya tumbo chini ya kitovu au mgongo.
5. Mkojo kuonekana kuwa wenye rangi ya damu au usaha.
6. Kutokwa na uchafu wenye harufu sehemu za siri, hasa tatizo hili linapokuwa la muda mrefu.

MADHARA YA U.T.I
Vimelea wa U.T.I wanapoingia sehemu ya uke, wanaweza kushambulia na kuharibu sehemu zifuatazo:
1. Tabaka la juu la mlango wa kizazi na kusababisha uvimbe wa shingo ya kizazi.
2. Kuziba kibofu cha mkojo au mirija ya mkojo.
3. Kuharibu figo za mhusika.

MATIBABU
Matibabu mara nyingi hupatikana katika vituo vya kutolea huduma za Afya kama Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali. Lakini mara nyingi tatizo haliishi au hujirudia kutokana na dawa nyingi zinazotumika huenda kuwatuliza tu bakteria hivyo baadae kuanza kusumbua tena.