December 29, 2017

Ukiona kiumbe hiki ufukweni, kimbia.

Hauwezi kutegemea matatizo yeyote uwapo umetulia ufukweni, ila ni vyema kujua ni vitu gani vya kujikinga navyo ukiwa kwenye fukwe za bahari.

Mara nyingine matatizo yanakuja katika hali ya kuvutia. Kama haujui ni nini,unaweza kufanya kosa kubwa kuvutiwa na uzuri wa kiumbe usichokijua.

Naamini habari hii itakusaidia kujiepusha na maumivu ya bahati mbaya utakayoweza kuyapata bila kujua. Kama ulishawai kumuona mnyama wa namna hii ni vizuri ku-share na watu ili nao wapate kujua.

Mnyama ufaamika kwa jina la Portuguese man of war, yupo kama Jellyfish ila sio jelly fish, ana miguu kama kamba zenye urefu wa 30-feet na wengine imefika hadi 165-feet.

Ni kama viumbe vinne vinaishi pamoja, kila kimoja kina kazi yake, kuanzia jinsi anavyotembea hadi uzaaji wao. Akikugusa au akikuuma anaweza kukusababishia ku-paralyze na maumivu makali hata kifo.

Kitu kingine kibaya katika huyu mnyama mwenye kuvutia ni kwamba hatari yake inaweza kudumu majuma kadhaa baada ya kutoka kwenye fukwe.

Unachotakiwa kufanya usimguse mnyama huyu ukimuona ufukweni na wala usiguse njia haliyopita, kwa bahati mbaya ukigusa kwa kutokujua nenda hospitali mara moja.

Source: DailyMail