January 11, 2018

Aina 8 za watu kwenye familia. (part one)

1. Anayejali.
Kila familia inahitaji aina hii ya watu angalau hata mmoja tu. Huyu ni mtu anayeweka mahitaji ya wengine mbele kisha mahitaji yake yanafuta nyuma mara zote hutaka kujua hali ya wenzake, maendeleo yao na kama wanahitaji msaada wa aina yoyote ile. Anayejali ni aina ya mtu ambaye atakuletea supu na mtori wakati unaumwa, na yuko tayari kusikia hadithi za maigizo yako na mpenzi wako mliyeachana(Drama).

2. Mtawala.
Watawala siku zote wana maoni na wanapenda kila kitu kiende sawa sawa na matakwa yao, kwanzia chakula, uvaeje, wikendi mwende wapi kutembea kama familia. Mara nyingi wanakela, lakini ni watu wa muhimu sana katika kuweka mipango na inasemeka aina hii ya watu ni wapangaji bora wa mipango. Kukiwa na sherehe, harusi ama matukio makubwa ya kifamilia watawala ni watu wa kuwategemea.

3. Wapenda amani/wapole.
Familia zote zina migogoro mara kwa mara, na hapo ndio ambapo umuhimu aina hii ya huonekana. Wao ndio wanaosuruhiisha ugomvi kati ya wanafamilia ambayo walikosena, wanajua namna ya kutengeneza hali ya utulivu kwa sababu ya heshima ambayo imetokana na upole wao. hawapendi kuona umoja wa familia ukiondoka na  kuamini ni bora kuwa na furaha kuliko kuwa sahihi.

4. Mzee wa fujo.
Watu wengine hawawezi kujizua kuharibu vitu. Hii ni aina ya watu ambao atakuja chumbani ama nyumbani kwako na atajisikia kama nyumbani na wakati anaondoka sebuleni ama chumba chako kitakuwa kama jalala.    Ikiwa unaishi na aina ya mtu, unapaswa kukubali mapema kwamba nyumba yako haitakuwa katika hali ya usafi tena. Kwa bahati mbaya sana, aina ya watu huwa hawajui kama  wamekosea.

5. Mkimya
Hii ni aina ya watu ambayo kamwe huwezi kujua wanachowaza. Mtajadiliana kama familia, mtapiga stori na kuongea lakini yeye amekaa kimya. Mara nyingi aina hii watu hupenda kukaa peke yao tena wote mnaweza kuwa sebuleni yeye kajifungia chumbani kwake. 

6. Mzembe.
Unajua kwamba kuna yule binamu ambaye atakaa tu kwenye sofa asubuhi mpaka jioni bila kufanya chochote akiwa na furaha tu na ikitokea ameinuka ni muda wa chakula ama kaenda kuchukua kitu kwenye friji ama natafuta chaji ya simu. Inashangaza sana mtu anaweza kukaa kwa masaa bila kufanya chochote. Ni vizuri kwa sababu familia haiwezi kukamilika bila kupata mtu mmoja ambaye yuko vizuri kwenye kutokufanya chochote.

7. Mtaalam wa mapishi
Nani ni mtaalam wa mapishi kwenye familia yenu? Aina ya watu hujaribu mapishi mapya kila siku na kuwasukumia wengine chakula hicho. Kama ni mpishi mzuri mnabahati sana lakini kama ni mpishi mbaya, mtaishi kwa kukimbia vyakula vya majaribio kila siku.

8. Kipaza sauti.

Huyu hawezi kukaa kimya, tena wana kelele. Wao huwa na maoni, na kelele, na wanataka kuhakikisha kwamba kila mtu anajua kile wanachofikiri. Saa zingine huonekana kama watu wa ajabu lakini mara nyingi wanafurahisha sana, wanapenda kujichanganya na wanajua kula bata vizuri.